Dirisha la maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2022/2023 kufunguliwa Kesho julai 19

Kasomi

JT Founder
Dirisha la maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2022/2023 litakuwa wazi kwa muda wa siku 70 kuanzia Julai 19 hadi Septemba 30 mwaka huu, hivyo tunawasihi wanafunzi waombaji wasome mwongozo kabla ya kuomba mkopo kwa kuwa ndiyo unataja sifa, vigezo na utaratibu wa kuomba mkopo.

“Uzoefu unaonesha kuwa wanafunzi waombaji wamekuwa hawazingatii taratibu wakati wa kufanya maombi. Tunawasii mzingatie maelekezo ya mwongozo. Wakati wa dirisha la maombi kumekuwepo na changamoto nyingi zinazojitokeza kwa waombaji”, alisema Prof. Mdoe.

Katika mwaka wa masomo 2022/2023, Serikali imetenga kiasi cha TZS 573 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo na skolashipu kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini.

Pia soma
 

Similar threads

Back
Top