Advertise here

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza nafasi za kazi kwa watendaji watakaosimamia Uchaguzi

Kasomi

JT Founder
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuendesha uchaguzi wa Rais na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na madiwani kwa Tanzania Bara, mwaka 2025. Katika kutekeleza jukumu hilo, Tume inatangaza nafasi za kazi ili kupata Watendaji watakaosimamia zoezi hilo kwa Tanzania Zanzibar. Kazi hizo ni zifuatazo:-

1. Mratibu wa Uchaguzi (Nafasi moja Unguja na Nafasi moja Pemba)
Majukumu:
(i) Kuratibu habari na taarifa mbalimbali za uchaguzi.
(ii) Kuratibu upatikanaji wa vifaa na nyenzo zinazohitajika katika kufanikisha Uchaguzi.
(iii) Kuwa kiungo kati ya Tume, watendaji wa shughuli za uchaguzi katika Wilaya/Majimbo na wadau.
(iv) Kushirikiana na kushauriana na wasimamizi wa uchaguzi waliopo katika eneo lake.

Sifa za Mratibu wa Uchaguzi:

(i) Awe raia wa Tanzania.
(ii) Awe Mtumishi wa Umma.
(iii) Awe na Shahada au Stashahada ya Juu au Stashahada katika fani yoyote.
(iv) Awe mwadilifu na mwaminifu.
(v) Awe mkazi wa eneo husika (Pemba au Unguja).
(vi) Awe tayari kujituma na kuweza kufanya kazi bila ya usimamizi wa karibu.
(vii) Awe na uzoefu katika masuala ya Uchaguzi/Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
(viii) Awe hajawahi kutiwa hatiani katika shauri la nidhamu au kosa lolote la jinai na kuadhibiwa kwa kifungo kinachozidi miezi sita (6).
(ix) Hajawahi kuwa kiongozi wa chama cha siasa.

Msimamizi wa Uchaguzi (Nafasi moja kwa kila Wilaya)

Majukumu

(i) Kuratibu na kusimamia shughuli za uchaguzi katika Wilaya yake.
(ii) Kusimamia na kufuatilia utendaji kazi wa watendaji wa uchaguzi chini yake.
(iii) Kutunza vifaa vya uchaguzi katika Wilaya husika.
(iv) Kusimamia matumizi ya fedha za uchaguzi.
(v) Kushirikiana na kushauriana na Maratibu wa uchaguzi katika kufanisi kwenye shughuli za uchaguzi.
(vi) Kuandaa taarifa ya mwendo wa hatua za uchaguzi kwa kuzin.
(vii) Kuandaa taarifa ya mwendo wa hatua za uchaguzi kwa kuzin maelekezo ya Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi.
a) Msimamizi wa Uchaguzi

(i) Awe raia wa Tanzania.
(ii) Awe mtumishi wa Umma.
(iii) Awe na Shahada au Stashahada ya Juu au Stashahada katika yoyote.
(iv) Awe mwadilifu na mwaminifu.
(v) Awe tayari kufutuma na kuweza kufanya kazi bila ya usimamizi karibu.
(vi) Awe na uzoefu katika masuala ya uchaguzi/ uandikishaji wa Daft.
(vii) Awe hajawahi kutiwa hatiani katika kosa la nidhamu au kosa la jinai na kuadhibiwa kwa kifungo kinachozidi miezi sita (6).
(viii) Hajawahi kuwa kiongozi wa chama cha siasa.

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo (Nafasi tatu kwa Jimbo)

Majukumu
(i) Kuwa kiungo kati ya Jimbo na Wilaya.
(ii) Kusimamia shughuli zote za uchaguzi katika Jimbo husika.
(iii) Kusimamia msimamizi wa uchaguzi katika masuala yote ya uchaguzi za Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi

Ngazi ya Jimbo
(i) Awe raia wa Tanzania.
(ii) Awe ni mtumishi wa umma.
(iii) Awe na Shahada au Stashahada ya Juu au Stashahada katika yoyote.
iv) Awe tayari kujituma na kuweza kufanya kazi bila ya usimam karibu.
(v) Awe na uzoefu katika masuala ya uchaguzi/uandikishaji wa Kudumu la Wapiga Kura.
(vi )Awe muadilifu na mwaminifu.
(vii) Awe hajawahi kutiwa hatiani katika shauri la nidhamu au kos la jinai na kuadhibiwa kwa kifungo kinachozidi miezi sita (6).
(viii) Hajawahi kuwa kiongozi wa chama cha siasa.

Mwombaji katika nafasi husika aainishe nafasi anayoiomba Wlaya au Jimbo analotaka kufanyia kazi na aambatnishe vyeti vya noja na maelezo ya taarifa binafsi (CV).

Maombi hayo yatapc anzia tarehe 03 Aprili, 2025 hadi tarehe 23 Aprili, 2025 saa 9:30 Alasiri.
rua zote zielekezwe kwa:

Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,
Ofisi ya Zanzibar,
Mtaa wa Maisara,
SLP. 4670,
Zanzibar.

MUHIMU: Maombi yote yatapokelewa katika Ofisi za Tume Huru ya T ya Uchaguzi zilizopo Maisata kwa upande wa Unguja na Chake Chake (Mtaa wa Miembeni) kwa upande wa Pemba.
 

Similar threads

Back
Top