Advertise here

CHADEMA Yakosa sifa ya kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025

Kasomi

JT Founder
1744455128528.jpg

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amesema Chadema ambayo haikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi, haitashiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano.

Kanuni hizo zinasainiwa leo Aprili 12, 2025 na vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Serikali na (INEC) jijini Dodoma.

Vyama ambavyo vimehudhuria hafla hiyo ni ADC, Demokrasia Makini, DP, NRA, NLD, SAU,UDPD, ADA- TADEA, AAFP, CCM, CUF, ACT-Wazalendo, CHAUMMA, UMD, TLP, NCCR-Mageuzi, CCK, UDP.

Chanzo: EATV
 
Back
Top