Aina 3 za wanawake wanaopaswa kuwa makini kabla ya kupenda tena

Minga

New member
Kuna vitu mbali mbali vinavyoweza kutokea kwenye mahusiano na ukajikuta huwezi tena kuendelea na mahusiano hayo haijalishi ulipenda kiasi gani.

Kupenda ni zawadi.

Lakini kuna wanawake wanapenda tena bila hata kuwa na tahadhari, ni kama wanarudi kwenye majivu yaliyokuwa na moto bila kujua kama umezima au bado unawaka kwa ndani.

Hizi hapa aina tatu za wanawake wanaopaswa kuwa makini sana kabla ya kuruhusu moyo wao kufall in love tena kwa mwanaume mwingine...

1::Mwanamke aliyesalitiwa na mwanaume aliyemwamini sana.

Kuumizwa na mwanaume uliyempa kipaumbele kwenye kila kitu ni maumivu yasiyoelezeka.

Mwanamke huyu anahitaji muda wa kupona, na sio kuharakia kuwa na penzi jipya ili kupata faraja.

Maumivu ya usaliti yanaweza kumfanya asiweze kuwa na muda wa kuangalia utofauti kati ya mtu anayempenda kweli na mwenye tamaa zake binafsi, kwa sababu huwenda anahitaji faraja kwa wakati huo.

Kupenda kabla ya kupona ni kama kujenga nyumba juu ya kifusi cha nyumba iliyobomoka,itaanguka tu.

Usikimbilie mahusiano mapya kabla haujapona vidonda vya mahusiano yaliyopita.

2::Mwanamke anayejilaumu kwa kile kilichotokea.

Anajiambia labda angevumilia zaidi huwenda mambo yangekuwa sawa huko mbele.

Basi huyu mwanamke bado anaishi na majuto,hata akiingia kwenye husiano jipya hawezi kuona wala kufaidi uzuri wa hilo husiano jipya.

Majuto yatamtesa sana.

Dawa ni kuanza kujipenda na kujipa kipaumbele na kuacha kuishi makosa ya jana , na hali yako itakuwa sawa.

3::Mwanamke anayeogopa kuwa mpweke.

Upweke sio adui, bali ni fursa ya kujifahamu vizuri.

Watu wengi hujigundua kuwa wanauwezo fulani wanapojipa muda wa kuwa peke yao, so huu ni muda mzuri mno kujitafuta.

Mwanamke anayeogopa kukaa peke yake anaweza kumkubalia mwanaume yeyote alimradi tu awe na mtu. Hii ni hatari.

Maamuzi yanapofanywa kwa hofu badala ya maarifa kuna uwezekano mkubwa wa kuharibikiwa.

Kupenda kwa hofu ni tiketi ya maumivu ya siku zijazo.

Kupenda ni safari.

Safari yoyote inahitaji maandalizi.

Wanawake hawa watatu wanahitaji kutulia ili kujiponya na kujitambua kabla ya kuruhusu mtu mwingine kugusa moyo wao tena.

Maumivu ya zamani yasipotibiwa,huwa ni sumu kwa furaha ya baadaye.

E.M✍️
 
Somo moja makini Sana.
Hasa hiyo aina ya Kwanza ya wanawake nadhani hao ni hatari na ndo msemo wa "wanaume wote ni Mbwa" ndo ulipo tokea
 
"Bora tuachane ,au nimekuacha"Moja ya kauli za kipuuzi kwenye argument za wanawake Fulani Fulani!

Matokeo yake ukitafuta mbadala tu panic,vikao,hatua za ghafla n.k!

Hawa viumbe kuwaelewa kazi sana aiseh!
 

Similar threads

Back
Top