IAA Princess Yatwaa Ubingwa Ligi ya Wanawake Arusha

Kasomi

JT Founder
IAA PRINCESS YATWAA UBINGWA LIGI YA WANAWAKE ARUSHA
1000709462.jpg

Timu ya soka ya wanawake ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA Princess) imetwaa ubingwa wa Ligi ya Wanawake ngazi ya Mkoa wa Arusha baada ya kuifunga Emayani Queens kwa bao 1–0 katika fainali iliyopigwa Mei 24, 2026 katika Uwanja wa Barafu, Mto wa Mbu wilayani Monduli.

IAA Princess walipata ushindi huo muhimu kupitia mchezo uliokuwa na ushindani mkali, uliowawezesha kutwaa taji hilo la mkoa na kuandika historia mpya katika michuano hiyo iliyoanza Machi 2026 na ikishirikisha timu tisa mkoani Arusha.

Ushindi huu umeipa IAA Princess tiketi ya kushiriki Michuano Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (WRCL).
 

Similar threads

Back
Top