Advertise here

Utofauti wa Supp, Carry, Resit na Disco

Kasomi

JT Founder
Utofauti wa supp, carry, resit na disco pamoja na sababu za kila hali.

1. Supp (Supplementary Exam)

- Supp ni mtihani wa ziada au wa kurudia, ambao mwanafunzi anapewa fursa ya kufanya mitihani tena baada ya kushindwa kufaulu somo au masomo kadhaa katika mitihani ya kawaida. Katika hali hii, mwanafunzi anakuwa na alama za chini kuliko kiwango kinachohitajika, lakini anapata nafasi ya kufanya mtihani mwingine ili kujaribu kupandisha alama zake.
Mfano baadhi ya Vyuo au level fulani Mwanafunzi anaweza pata Supp akishindwa kufikisha alama 40 au 50 hivyo ata Supp kulingana na Chuo husika

Sababu za Hali ya Supp
- Alama za chini: Mwanafunzi anakuwa na alama za chini (kwa mfano, 39 au 49 ya alama za ufaulu yaan 40 au 50) ambazo hazikidhi kiwango cha kufaulu kinachohitajika Katika Vyuo vingi ngazi ya diploma na certificate ufaulu ni Alama 50 Wakati bachelor degree ufaulu ni 40.
- Ufinyu wa muda au maandalizi: Mwanafunzi anaweza kushindwa kutokana na kukosa muda wa kutosha kujitayarisha kwa mtihani wa awali, labda kwa sababu ya masuala ya kibinafsi au ya kifamilia.
- Kukosa kuelewa somo: Ingawa mwanafunzi amefanya bidii, inaweza kuwa ni kwamba alikosa kuelewa masomo kwa undani wa kutosha.

2. Carry (Carry Over)

Maelezo ya Hali ya Carry

- Carry inatokea pale mwanafunzi anaposhindwa kufaulu mtihani wa Supp. Hii inamaanisha kwamba mwanafunzi anaendelea na mwaka mwingine bila kupandishwa daraja hadi atakapofaulu masomo ambayo alishindwa. Mwanafunzi akiwa na carry ya masomo fulani, hawezi kwenda mbele kwenye hatua nyingine za masomo.
Hivyo Carry inaruhusu kuendelea na level nyingine/Mwaka mwingine huku ukiwa na mzigo wa Somo/masomo mengine. Mfano unaweza kuingia Mwaka wa Pili lakini ukawa na masomo au somo mwaka wa kwanza ambayo utafanya kipindi cha mitihani ya jumla

Sababu za Hali ya Carry
- Kushindwa kufaulu Supp: Ikiwa mwanafunzi alifanya mtihani wa ziada lakini hakufanikiwa kufaulu, basi anakuwa na carry.
- Kutokuwa na mipango bora ya masomo: Wanafunzi wanaoshindwa kupanga ratiba ya kujisomea vizuri au kuwa na nidhamu ya kujifunza mara nyingi hujikuta katika hali ya carry.
- Masuala ya kifamilia au kiafya: Wanafunzi wanaokutana na changamoto za kibinafsi au kiafya wanapata shida katika kujitolea kwa masomo, hivyo kuchangia kushindwa katika mitihani.

3. Resit (Repeating Module yaani RM)

Maelezo ya Hali ya Resit

- Resit ni hali ya mwanafunzi kurudia mtihani wa somo analoshindwa kwa kuanza kusoma upya level husika na kufanya kazi zote za darasani yaani Coursework.
Baadhi ya vyuo hii ni sawa na Repeating Module (RM) Hii ni sawa na mtihani wa ziada, lakini ni tofauti na Supp kwa sababu Resit inaweza kutumika kwa sababu mbalimbali kama vile mwanafunzi kutohudhuria mtihani wa awali au kutokamilisha mahitaji ya mtihani.
Pia Mwanafunzi anaweza Resit kwa kushindwa kufaulu Supp Katika baadhi ya level hivyo hawezi carry Bali ata Resit. Mfano Ukiwa unaingia Mwaka wa Tatu kwa level ya degree na ukashindwa kufaulu Supp hapo hauta Carry bali uta Resit.
Pia Mwanafunzi anae Weza kuresit ni yule hana sifa za Ku carry kulingana na level husika mfano kuingia NTA Level 5 au 6, na NTA Level 8

Sababu za Hali ya Resit
- Kukosa mtihani (absent): Ikiwa mwanafunzi alikosa mtihani bila ruhusa, atapewa fursa ya kufanya resit ili kutoa mtihani huo.
- Kufeli mtihani: Mwanafunzi anayeshindwa mtihani wa kawaida anaweza kutakiwa kufanya resit kwa lengo la kufaulu somo hilo na kuendelea na masomo yake.
- Kutokamilisha mahitaji ya somo: Wanafunzi wanaoshindwa kuwasilisha kazi za darasani, ripoti, au kufanya utafiti wanaweza kulazimika kufanya resit ili kukamilisha mahitaji ya somo.

4. Disco (Discontinuation)

Maelezo ya Hali ya Disco

- Disco ni hali mbaya zaidi ambapo mwanafunzi anaondolewa kabisa kwenye chuo kutokana na kushindwa kufaulu zaidi ya nusu ya masomo au kufeli zaidi ya supp mbili. Pia, wanafunzi wanaoshindwa kufikia viwango vya nidhamu au kushindwa kufanya mitihani bila ruhusa wanaweza kuondolewa chuoni.

Sababu za Hali ya Disco
- Kufeli zaidi ya nusu ya Masomo Katika Mwaka wa Masomo (baadhi ya vyuo mfano Una jumla ya Masomo 12 kwa Mwaka husika na uka Supp Masomo 7 hiyo ni Disco)
-Kushindwa kufanya Mitihani wa Final Examination, Supp, Carry au Resit pasipo taarifa maalumu au sababu ya msingi
- Kufeli zaidi ya Supp 2 yaani Carry 3 :) Ikiwa mwanafunzi amefeli masomo zaidi ya 2 ya Supplementary yaani masomo (au kulingana na vigezo vya chuo) au kufeli zaidi ya supp mbili yaani baada ya kufanya Supp anafeli tena Supp 3, anakuwa katika hatari ya kuondolewa chuoni.
- Kushindwa kufaulu mtihani wa Resit mara mbili.
Yaani amefanya resit ya Kwanza aka feli, akafanya resit ya pili akafeli tena hiyo ni Disco
- Kutokufuata kanuni za nidhamu: Matendo kama kufanya mitihani bila ruhusa, kufanya udanganyifu kwenye mitihani, au kutofuata maadili ya chuo yanaweza kusababisha mwanafunzi kufukuzwa.
- Kukosa kufanya kazi za field report au project ripoti: Ikiwa mwanafunzi hakufanya kazi za utafiti, ripoti, au alishindwa kutoa maandiko muhimu kwa ajili ya somo, huenda akaondolewa kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya masomo.
- Kutokuwa na juhudi za kutosha: Mwanafunzi anayeshindwa kwa mara kwa mara kufaulu au kuweka juhudi za kutosha katika masomo yake anaweza kuondolewa chuoni kwa sababu anakuwa ameshindwa kufikia viwango vya kitaaluma na nidhamu vilivyowekwa.
-Hivyo unaweza Disco kwa swala la kinidhamu mfano kukamatwa ukivunja Kanuni Za mitihani, kushindwa kufanya Mitihani bila ruhusa
 
Back
Top