Advertise here

Utofauti wa Domain na Hosting

Kasomi

JT Founder
Je, Unajua Tofauti Kati ya Domain na Hosting?
Watu wengi wamekuwa wakichanganya kati ya domain na hosting, lakini hizi ni vitu viwili tofauti vinavyofanya kazi kwa pamoja ili kuwezesha tovuti kuonekana mtandaoni.
Blue and Yellow Minimalist Website Development Instagram Post_20250323_031441_0000.png

1. Domain ni nini?
Domain ni jina la tovuti yako – mfano: jamiitalk.com au Kasomi.co.tz Hili ndilo watu huandika kwenye browser ili kufika kwenye tovuti yako. Ni kama anwani ya nyumba yako kwenye mitaa ya mtandaoni.

2. Hosting ni nini?
Hosting ni huduma ya kuhifadhi mafaili yote ya tovuti yako (picha, maandiko, video, nk). Ni kama nyumba yenyewe ambapo kila kitu kimehifadhiwa.

Tofauti kati ya Domain na Hosting kwa ufupi:

Domain ni jina, Hosting ni hifadhi.

Domain huonyesha wapi pa kwenda, Hosting huonyesha nini kiko huko.

Domain unaweza kuimiliki bila tovuti, Hosting haiwezi kufanya kazi bila domain.

Domain huuzwa na registrars, Hosting huuzwa na hosting providers.

Ukiwa na domain tu = unayo anwani.
Ukiwa na hosting tu = una nyumba bila anwani.
Ukiwa na vyote viwili = tovuti yako iko hewani!

Kwa hiyo kama unataka kuwa na tovuti kamili, unahitaji VYOTE VIWILI – Domain + Hosting.
 
Back
Top