Kasomi
JT Founder
Sanamu ya shaba ya Melania trump karibu na mji alikozaliwa nchini Slovenia imetoweka, miaka mitano baada ya kuwekwa mahali ilipokuwa sanamu ya mbao iliyoharibiwa na kuchomwa moto
Polisi wa Slovenia wamesema kwamba walikuwa wamearifiwa kuhusu wizi katika kijiji cha Rozno, ambapo sanamu hiyo ilikuwa, siku ya Jumanne.
Maafisa "walifanya ukaguzi wa eneo la uhalifu na kukusanya taarifa," msemaji wa polisi Alenka Drenik Rangus alisema katika taarifa Ijumaa. "Jaji mchunguzi na mwendesha mashtaka wa wilaya waliarifiwa kuhusu wizi huo."
Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa na mamlaka.
Picha zilizochapishwa katika vyombo vya habari vya Kislovenia zinaonyesha sehemu kubwa ya sanamu hiyo ikiwa imekatwa kwa msumeno, na kuacha tu miguu na vifundo vyake vikiwa vimeunganishwa kwenye shina la mti ambalo ilisimikwa.
Sanamu hiyo ilikuwa kando ya mto karibu na Sevnica, mji mdogo wa kupendeza ulio umbali wa kilomita 90 (maili 56) mashariki mwa mji mkuu wa Slovenia Ljubljana.
Kabla ya sanamu hii ya shaba kuibiwa, sanamu yake asili ya mbao ilichomwa moto mnamo Julai 2020 na waharibifu. Ilichomwa vibaya, kisha ikaondolewa kutoka kwenye kilele chake kabla ya kuonyeshwa kwenye jumba la sanaa katika mji wa Slovenia wa Koper baadaye mwaka huo na kwenye maonyesho huko Croatia mnamo 2023
Miezi minne baada ya Melanija Knavs kurudi katika makao ya White House kufuatia kurudi madarakani kwa Rais Trump, sanamu lake kubwa lililokuwepo katika ukingo wa mto wa Sava limetoweka kutoka mji wa Sevnica alikozaliwa huko nchini Slovenia.
Kilichosalia kwenye sanamu hiyo kubwa ya shaba ni miguu na kigutu cha mti chenye urefu wa mita mbili ambapo sanamu hiyo ilikuwa ikisimama.
Hii sio mara ya kwanza kwa tukio la aina hii la kumpa Melania Trump heshima lililoishia na mwisho mbaya huko Sevnica,Sanamu ya kwanza ilizinduliwa mnamo Julai 2019.
Polisi katika eneo hilo wanauchukulia mkasa huo wa kutoweka kwa sanamu ya Melania kama wizi na wameidhinisha uchunguzi.
Chanzo: EastAfricaTV