Kaka wa Tundu Lissu kuzikwa baada ya hukumu ya Lissu

Kasomi

JT Founder
1000975120.jpg

Familia ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imetangaza kifo cha kaka yao, Wakili Alute Lissu Mughwai, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili, Novemba 1, 2026, katika Hospitali ya Selian mkoani Arusha.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Dkt. Vincent Mughwai amesema marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu. Katika siku za hivi karibuni, hali yake ilizorota na kulazimika kulazwa katika Hospitali ya Selian, ambako alifariki dunia majira ya saa nane usiku.

Dkt. Vincent amesema familia imepokea taarifa za kifo hicho kwa huzuni kubwa, ikizingatiwa mchango na nafasi muhimu aliyokuwa nayo marehemu ndani ya familia, hususan kama msemaji wa familia na mmoja wa viongozi wakuu wa ukoo.

Ameeleza kuwa mazishi yanatarajiwa kufanyika mkoani Singida, hata hivyo, tarehe rasmi ya mazishi itatangazwa baada ya familia kukutana na kukamilisha taratibu zinazohusika.

Aidha, amesema familia inapanga kusogeza mbele shughuli za mazishi ili kutoa fursa kwa ndugu, jamaa na marafiki kushiriki katika usomaji wa hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu, unaotarajiwa kufanyika Ijumaa, Novemba 6, 2026, jijini Dar es Salaam.

Zaidi soma hapa

Chanzo: East Africa TV
 
Back
Top