Kasomi
JT Founder
KUDOS, RADIO ONE STEREO
Mwaka 1993, Mfanyabiashara Mzalendo Reginald Abraham Mengi alianzisha kituo binafsi cha redio nchini kiitwacho Radio One.
Kuanzishwa kwa kituo hicho, kikitanguliwa na kituo cha kwanza binafsi nchini cha Radio Tumaini, kulileta mapinduzi makubwa katika sekta ya habari.
Watangazaji nguli waliochukuliwa kutoka Radio Tanzania (sasa TBC Taifa), Charles Hillary (R.I.P), Mikidadi Mahmoud na Julius Nyaisanga, wakafanya makubwa yaliyopelekea Radio One kupendwa sana.
Kazi nzuri ya wakongwe hao ikaifanya Radio One kuwa 'injini' ya kuzalisha watangazaji wengi mahiri kuliko kituo chochote kingine cha habari nchini wakati huo.
Radio One ikawa kama ndiyo redio ya Taifa. Habari makini na mahiri za kitaifa na Kimataifa zikaonekana kusikilizwa na kuaminiwa zaidi kupitia kituo hiki.
Ili kudhihirisha umahiri wake, Watangazaji wengi wa Radio One wakachukuliwa na redio za Kimataifa kama BBC, DW, VOA, nk kwa ajili ya kuuhabarisha ulimwengu.
Nje ya utangazaji, waandishi wengi waliopita Radio One wamefanikiwa kupata uongozi katika nafasi mbalimbali za kisiasa na kitaaluma, kitaifa na Kimataifa.
Pamoja na uwepo wa redio nyingi nchini, Radio One itabaki kuwa redio iliyotoa mchango mkubwa sana kwa Taifa katika miaka 32 ya kuanzishwa kwake.
Pichani ni baadhi ya watangazaji na Ma-Dj's waliopita kwenye mikono ya Radio One Stereo, ambao kwa hakika kupitia kituo hicho wamefanya mambo makubwa sana.
Mstari wa kwanza juu kutoka kushoto ni: Amina Mollel, Rukia Mtingwa, Deo Mshigeni, Masoud Masoud, Frola Nducha, na Sebastian Maganga.
Mstari wa pili kutoka kushoto ni: Millard Ayo, Vicky Msina, Dj Fast Eddy, Basil Mbakile, Dj Ommy (RIP) na Taji Liundi.
Mstari wa tatu kutoka kushoto ni: Moses Justin (RIP), Neema Diwani, Abdallah Mwaipaya, Regina Mwalekwa, Dj John Dilinga, na Rose Chitala.
Mstari wa nne kutoka kushoto ni: Misanya Bingi (RIP), Flora Nducha, Taji Liundi, Maulid Kitenge, Abubakar Sadik, na Isaac Muyenjwa Gamba (RIP).
Mstari wa tano kutoka kushoto ni: Mike Pesambili Mhagama, Sunday Shomari, Godwin Gondwe, Abdallah Majura, Abubakar Liongo, na Sostenes Ambakisye.
Mstari wa sita kutoka kushoto ni: Mikidadi Mahmoud, Julius Nyaisanga, Charles Hillary, Ahmed Kipozi, Janeth Sostenes Mwenda, na Betty Mkwasa.
Baadhi ya watangazaji ambao wamepita Radio One na hawapo pichani ni: Leila Muhaji, Blandina Mungezi, Suzan Mungi, Monica Mfumia, Deogratius Rweyunga, Asia Mohamed na wengine wengi.
Mungu awapumzishe kwa amani wale wote waliotangukia mbele ya haki, na azidi kuwapa nguvu, na afya njema wote waliowahi kupitia kituo hiki.
Hongereni sana Radio One Stereo kwa Sasa ina miaka 32 ya Kutuhabarisha, Kutuelimisha na Kutuburudisha. Tunawapenda na mzidi kubarikiwa.!
Credit: Kado cool