February 13 Ni Maadhimisho ya siku ya Radio Duniani

Kasomi

JT Founder
FEBRUARY 13 NI MAADHIMISHO YA SIKU YA RADIO DUNIANI.
1739425551619.jpg

JamiiTalk inaungana na Vyombo vya Habari kote Ulimwenguni Kuadhimisha Siku ya Radio Duniani.

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO lilianzisha Siku ya Radio Duniani mnamo Mwaka 2012 mara baada ya Baraza Kuu la Unesco kutambua umuhimu wake na mwaka uliofuata Umoja wa Mataifa ukatambua kama Siku ya Radio Duniani.

Hata hivyo kwa kuthibitisha kuwa, kila tarehe 13 Februari itakuwa inaadhimishwa kutokana na kwamba, tarehe hiyo mwaka 1946 ndipo ilianzishwa Radio ya Umoja wa Mataifa.

Ni katika kutumia chombo hiki cha Mawasiliano na msingi wa kutoa habari ambayo inasaidia kukuza uhuru wa kujieleza na usawa wa kila kitu.

Radio iweze kutoa mchango katika mijadala ya kidemokrasia kwa njia ya kubadilishana mawazo kati ya Watangazaji na Wasikilizaji.

Kwa maana hiyo Radio imekuwa ni nguzo kuu ya kijamii inayoendelea na iliyo endelea Duniani kote.
 
Back
Top