Kasomi
JT Founder
Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Aziz Ki baada ya kujiunga na Wydad Casablanca ya Morocco, mshahara wake kwa mwezi utakuwa ni Dola40,000, wastani wa Sh108 milioni.
Inaelezwa katika usajili huo, pia Aziz Ki amelamba Dola150,000 , wastani wa Sh405.2 milioni ya kusaini, huku Yanga SC ikichukua Dola350,000, wastani wa Sh945.4 milioni.
Aziz Ki amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Wydad hivi karibuni na alikuwa ameongozana na mkewe Hamisa Mobetto katika kufanikisha dili hilo kubwa zaidi katika maisha yake ya soka.
Ikumbukwe Wydad wameharakisha usajili huo ili akacheze michuano ya mipya ya FIFA ya Kombe la Dunia la Klabu inayotarajiwa kuanza Juni 14 hadi Julai 13 nchini Marekani ikishirikisha timu 32 kutoka mabara sita.
Ikumbukwe timu nne kutoka Afrika ambazo zinashiriki michuano hiyo ni Al Ahly ya Misri, Esperance ya Tunisia, Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini na Wydad Casablanca ya Morocco ambayo mchezo wa kwanza itacheza dhidi ya Man City.
Chanzo: JamboMail