Advertise here

CBE na Niajiri Platform LTD waingia makubaliano

Mtata

Member
FB_IMG_16510664343503451.jpg

Leo 27/04/2022 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema amekutana na Bi. Lilian Secelela Madeje ambae ni Mwasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Niajiri Platform LTD na kutia Saini Mkataba wa Makubaliano (MOU) ya Ushirikiano baina ya CBE na Niajiri.

Bi. Secelela alisema "Niajiri Platform LTD inampa nafasi mwanachuo aliye hitimu masomo yake kuweza kupata ajira kwa urahisi, lakini sio tu kumtafutia ajira pia mwanachuo atapata nafasi ya kuendelezwa na kupewa ujuzi kwenye mambo mbali mbali mfano Kujitambua, Jinsi ya kuwawasiliana kazini, Uandishi Bora wa CV, kuandaliwa kwaajili ya Usaili na kupata Elimu ya Ujasiriamali".
FB_IMG_16510664429158995.jpg
 

Similar threads

Back
Top