Mwongozo kwa watumiaji wa JamiiTalk | Sheria, kanuni na taratibu.

Status
Not open for further replies.

JamiiTalk

Official Support Account

Ni nani anayeweza kutumia JamiiTalk?​


JamiiTalk ni jukwaa huru ambapo kila mtu anaweza kutumia pamoja na kushiriki katika Mijadala (Kwa member waliojisajili). Watu wanapotetea maoni na vitendo vyao, jumuiya yetu inakuwa salama na inawajibika zaidi. Kwa sababu hii, ni lazima:

1- Utumie jina (lile ambalo unalolitumia katika maisha ya kila siku au Jina lisilojulikana yaani anonymous name).

2- Ni lazima kuweka barua pepe yako (email) pamoja na neno siri lako (password)

3- Uunde akaunti moja tu (yako binafsi)

4- Weka Taarifa zako za hiyari kama Tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa pamoja na Mahali

NB: Usisambaze nenosiri lako, kutoa ufikiaji kwa wengine kwenye akaunti yako ya JamiiTalk, au kuhamisha akaunti yako kwa mtu mwingine yeyote (bila kibali chako).
Tunajaribu kufanya JamiiTalk kupatikana kwa ujumla kwa kila mtu, pia unaweza kusoma na kuperuzi Mtandao wetu hata kama hujajisajili, lakini hutoweza kushiriki kwenye mijadala kama huna account ya JamiiTalk (kushiriki kwenye mijadala lazima ujisajili na JamiiTalk).
lakini huwezi kutumia JamiiTalk kama:

-Una umri mdogo wa kisheria katika nchi yako wa kutumia Mtandao.

Sheria za JamiiTalk.

Mtandao wa JamiiTalk ni mtandao wa kijamii ambao unakutanisha Jamii ili kujadili mambo mbalimbali, hivyo ukiwa katika mtandao huu hupaswi;

1- kusambaza/kuandika maudhui au habari za uongo.

2- picha, video au maudhui ya ngono hayaruhusiwi

3- Matangazo ambayo yanakiuka sera zetu au sera za serikali hayaruhusiwi.

4- Unyanyasaji wa aina yeyote hauruhusiwi (iwe kwa jamii au kwa Washiriki wenzetu).

5- Maudhui ya Matangazo bila ruhusa yataondolewa (ukitaka kutangaza wasiliana na uongozi wa JamiiTalk)

6- Viungo vya matangazo haviruhusiwi (Advertising Hot Links) mfano blog, website, kurasa za mitandao ya kijamii.

7- Utani unao chukiza/ kukera hauruhusiwi (Member akikufanyia utani wa chuki au kukera unaweza report (kwa kubofya kitufe cha report Chini ya ujumbe au chini ya member na kuandika Sababu ya kureport) au uka mpuuza kwa kubofya kitufe cha Ignore

8- Huruhusiwi kumtaja au kumuanika member kwa majina yake halisi kama ameamua kutumia Jina lisilojulikana yaani anonymous name hata kama ukimfananisha (JamiiTalk inalinda Faragha za watumiaji wake)

9- Kuvaa uhusika wa mtu mwingine au kuingilia akaunti ya mtu: Usithubutu kuvaa au kujifanya wewe ni muhusika fulani ikiwa wewe siye. Usivae uhusika wa viongozi wa umma au mwanachama fulani au kutengeneza akaunti maalumu kwa dhumuni la kuwadhalilisha au kuwachafua wanachama wengine na wananchi wengine kwa ujumla.

10- Washiriki wanapaswa kutumia lugha ya kiungwana na kistaarabu ili kuhakikisha kuwa heshima na uvumilivu vinatawala katika mijadala.
JamiiTalk ipo kwa ajili ya kusaidia hivyo wahusika wasaidiane panapobidi badala ya kuchukizana au kutumia lugha isiyo faa.


Hivyo Kwa kukiuka sheria zetu Maudhui yataondolewa na muhusika atapewa onyo, lakini kwa sababu nyingine muhusika anaweza zuiwa kushiriki kwenye mijadala kwa muda (Ban)

Usitishaji au ukomeshaji wa akaunti

Tunataka JamiiTalk liwe eneo ambalo watu wanajihisi huru na salama kujieleza na kushiriki mawazo na hoja zao.
Ikiwa tutabaini kwamba umekiuka Masharti au Sera zetu kwa namna bayana, vibaya sana au mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na haswa Viwango vyetu vya Jumuiya, tunaweza kusitisha au kulemaza kabisa uwezo wako kufikia akaunti yako (Ban). Tunaweza pia kusitisha au kulemaza akaunti yako ikiwa umekiuka mara kwa mara haki za watu wengine au pale tunapohitajika kufanya hivyo kwa sababu za kisheria.

Pale ambapo tutachukua hatua kama hiyo tutakufahamisha na kukueleza kuhusu chaguo zozote ulizo nazo kuomba ukaguzi, isipokuwa ikiwa kufanya hivyo kutatuweka au kuwaweka watu wengine kuwajibika kisheria; kuiumiza jumuiya ya watumiaji wetu, kutia doa au kuingilia maadili au uendeshaji wa vyanzo, mifumo au Bidhaa zetu zozote, ambapo tumewekewa vikwazo kutokana na vizuizi vya kiufundi; au pale ambapo tumewekewa marufuku ya kufanya hivyo kwa sababu za kisheria.
Unaweza kujifunza zaidi kuhusu kile unaweza kufanya iwapo akaunti yako imelemazwa na jinsi ya kuwasiliana nasi iwapo unafikiria tumelemaza akaunti yako kimakosa.
Iwapo utafuta au tukilemaza akaunti yako, Masharti haya yatasitishwa kama makubaliano baina yako na sisi.

Kwa ukiukaji wowote unaweza wasiliana nasi kwa barua pepe au Ujumbe binafsi (PM) kwenda kwa Staff members, au bonyeza hapa kuwasiliana nasi CONTACT US

===
Karibu katika jukwaa huru.

JamiiTalk The Home of Learning. Let The Jamii Talk
 
Status
Not open for further replies.

Similar threads

Back
Top