john achila mukumwa
Member
Siyo sahihi kwa Mkristo kucheza gemu
Kucheza gemu kwenye komputa au simu ni sahihi? Mfano gemu ya mpira, vita, kupigana, karata, magari, pool-table, na mengineyo, je ni dhambi?
Kabla ya kujibu swali hili, ni muhimu kwanza kujua michezo hiyo kama ni sahihi kuishiriki au la.
Kwa mkristo aliyeokoka, hapaswi kushiriki michezo ya kupigana, iwe uwanjani kama ndondi, au vitani; iwe kwa nia ya fursa au burudani. Hii ni kwa sababu biblia inasema kushindana kwetu si juu ya damu na nyama, bali juu ya falme na mamlaka za mapepo katika ulimwengu wa roho (Waefeso 6:10-13); na vita vya kiroho dhidi ya mapepo si vya kujiburudisha au kujifurahisha.
Vile vile, mkristo hapaswi kucheza pool-table, kwa sababu ni mchezo wa ibilisi na unaochezwa na watu wasio na Roho wa Mungu. Ndiyo maana meza zake zipo maeneo yafanyikapo anasa kama vile disko, au baa. Huwezi kukuta pool-table kanisani.
Ni vizuri pia kufahamu kuwa michezo ya karata chimbuko lake ni upagani, yaani umataifa. Waanzilishi wake ni watu wa Asia (Uturuki), ambao walikuwa wanatumia vitu hivi kwa ajili ya kubashiri na kufanya michezo ifananayo na hiyo. Wakristo siyo wapagani. Je Wakristo wachanganye vilivyo vitakatifu na hivyo ambavyo wasio mjua Mungu huvitukuza?
Hivyo siyo sahihi kwa mkristo kucheza magemu katika kompyuta au simu au katika kifaa kingine chochote. Vivyo hivyo, hata michezo live, kama vile karata na bao, siyo sahihi mbele za macho ya Mungu.
Aidha, yapo magemu yaliyotengenezwa pasipo kuhusisha michezo ya damu na nyama. Hayo ndiyo hatari kabisa, kwa sababu yamebuniwa kutoka katika mambo yanayoendelea rohoni.
Kwa mfano, utaona kuna magemu ya nyoka. Joka linazunguka na kumeza vitu. Mambo haya hayapo katika ulimwengu wa mwili, lakini yapo katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu shetani anataka kuendeleza mahusiano kati yake na wanadamu hata kwa njia ya mwili; ndiyo yanakuja haya magemu.
Mtu anapocheza game la kumwongoza nyoka kumeza vitu, au anapocheza game la kukimbizwa na joka, au kukimbizwa na viumbe visivyojulikana, basi anashiriki na kuthibitisha mambo hayo katika roho.
Hivyo, maisha yake yataendeshwa na hayo maroho kwa kupenda au kutokupenda. Hata ndoto zake zitakuwa zinaweza kujaa hayo mambo.
Roho ya kupenda na kucheza magemu inaongezeka kwa kasi siku hizi za mwisho, na hasa kwa njia ya simu. Biblia inasema tusiipende dunia wala mambo yaliyomo duniani, kwani mtu akiipenda dunia hata kumpenda Baba hakupo ndani yake. Tusome kitabu cha Yohana:
1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”.
Pia, katika Wafilipi 4:8, Biblia inasema: 8 "Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo".
Kwa nini biblia inasema tusiipende dunia? Siyo kwamba dunia ni mbaya, siyo kwamba michezo ni mibaya, wala siyo kwamba kustarehe ni kubaya. Hapana. Vitu vyote hivyo siyo vibaya kama vikitumiwa ipasavyo. Ubaya ni kwamba tunaishi duniani kwa muda tu.
Mungu wetu hataki tupotee. Ndiyo maana anatuambia tukae mbali na mambo hayo ya ulimwengu. Sisi (watoto wa Mungu) ni sawa na mwanafunzi walioko shuleni, tena shule za bweni. Ni wasafiri tu wa hapa duniani. Tunatengeneza maisha yetu sasa, ili tuwe na maisha bora huko katika umilele unaokuja.
Hivyo kama ni starehe, basi tutazifanya sana katika hiyo mbingu mpya na nchi mpya inayotungojea huko mbeleni. Kama ni kufurahi, kama ni kuzurura, kama ni kucheza na kujiburudisha kwa jinsi tupendavyo, basi tutafanya sana katika hiyo Yerusalemu mpya, ambayo Mungu ametuandalia huko mbeleni.
Lakini sasa katika ulimwengu huu, siyo wakati wake. Hayo mambo ni ya wakati wa ulimwengu ujao, ambapo huko kutakuwa hakuna kusoma tena biblia wala kuhubiri, wala kufunga, wala hakutakuwa na majaribu tena, wala maumivu, wala kula kwa jasho, wala kujizuia. Hayo mambo hayatakuwepo kule. Kule itakuwa ni sehemu ya furaha, kufanikiwa na uhuru usio na kifani. Ndivyo maandiko yanavyosema.
Lakini Wengi wanasema ni ushamba kujinyima raha katika ulimwengu huu. Lakini hao hao, hawajui kuwa ni ushamba mkubwa zaidi kujinyima raha za umilele unaokuja huko mbeleni.
Hebu jiulize, ukifa leo, huko utaenda kuwa mgeni wa nani? Kumbuka mwanafunzi mwenye busara ni yule anayezingatia kilichompeleka shuleni. Siyo ushamba mwanafunzi kujizuia kuangalia movie ili atumie muda wake vizuri katika masomo. Wala siyo ushamba mwanafunzi anapojizuia kuzurura-zurura huku na huko, na badala yake muda wote unautumia kutafakari masomo, ili mitihani ikija, afaulu vizuri. Anajinyima hivyo vyote, kwa sababu anajua ni kwa faida yake mwenyewe, na ni kwa muda mfupi tu. Anajua kuwa siku akimaliza shule na kufaulu, atayafanya hayo sana na zaidi ya hayo.
Tunapaswa tuzingatie kwa sasa kile kilichotuleta duniani. Siyo ushamba kuukataa ulimwengu. Siyo kila kitu kinachokuja mbele yetu tukijaribu. Vingine vinatupotezea muda, vingine vinatuondoa katika dira ya wokovu, vingine vinaturudisha nyuma. Ni wajibu wetu kuenenda katika hii dunia kwa werevu.
Kwa kuhitimisha, mchezo wa karata haufai kwa mtoto wa Mungu. Utacheza karata kwa masaa mawili, lakini kushika biblia dakika tano huwezi. Utaangalia muvi series hata masaa manane, lakini biblia dakika 10 huwezi. Huoni kuwa kuna roho nyuma ya huo mchezo? Roho inayokufanya kutokuzingatia mambo ya msingi ya imani.
Aidha, michezo mingine hiyo hupoteza muda wa yeye achezaye, muda ambao heri angekuwa katika Neno la Mungu na maombi. Muda ambao ungetumia kumsifu na kumtukuza muumba wako.
Kucheza gemu, na mchezo huo kutokuwa sahihi mbele ya Mungu, ni mambo mawili tofauti. Hata kama watu wanapenda kucheza magemu hayo, haimaanishi kuwa ni sahihi mbele ya Mungu.
Kwa ujumla, Mkristo haruhusiwi kucheza magemu na michezo mingine kama vile karata na bao.
Hii ni kwa sababu mchanganyiko, kama ifuatavyo:
1. Chimbuko lake ni upagani, yaani kimataifa
2. Ni michezo ya ibilisi
3. Haipo katika ulimwengu wa mwili bali katika ulimengu wa roho.
4. Imejikita katika kuipenda dunia badala ya kumpenda Yesu.