Advertise here

Shahidi lyrics - Dizasta vina

Kasomi

JT Founder
Sing: Shahidi by Dizasta vina
1762414392137.jpg

Nilipanda kwenye jukwaa/
Watu walinishangaa/
Unadhifu wa meli haukufanana na nilivyovaa/
Kabla sijatoa salamu...
Walipoteza hamu ya kuburudika wengine wakaanza kusambaa/
Nilikuwa na nywele nyingi/
Zilionesha pia siku ni nyingi/
Tangu mara ya mwisho ziwekwe MAJI/
Wale matajiri waliosheheni kwenye viti/
Walicheka wakihisi mim chizi au mchekeshaji/

Waliokaribu pia wakaanza kunitunza pesa/
Na waliombali walijaribu kurusha fedha/
Kwa yote niliyowaeleza/
Hakuna aliyeyaweka kichwani wote walihisi kuwa nataka kuchekesha/

Walinitemea shombo kwa kejeli/
Wengine walihisi nalianzisha zogo kwenye meli/
Muonekano haukuyabeba maneno yangu hawakuamini niliposema kuwa chombo kina mushkeli/
Niliwaeleza kuwa kule ndani Kuna tundu dogo/
Linapitisha maji linazamisha chombo/
Waliendelea kujadili siasa na vibonzo/
Hakuna aliejadili kuhusu roho/
Za wasaka tonge wanyonge wasafiri daraja la tatu/
Hawakulipa PESA nyingi ila walikuwa ni watu/
Maji yalianza kuingia vyumbani mwao iliwekwa mipaka hivyo taarifa hazikufika katu/

Nilienda mpaka chumba cha sauti/
Nitoe tangazo kabla hatujakumbwa na mauti/
Mtoa sauti aliwataja matajiri/
Akiwapa sifa majina makubwa na saluti/

Niliwaambia wekeni glass chini mtege masikio/
Hizo kelele mnazosikia SI sherehe ni vilio/
Wakasema nimedata nataka kuanzisha vagi ilionesha wazi hawakuona mbeleni tishio/
Hata kwenye vyumba vya wasomi maarufu/
Vyeti walihodhi maradufu/
Niliwahoji kuhusu ubovu wa meli...
Wengi waliujua ubovu/
Lakini walisema haiwahusu/

Naapa haki nilienda kote/
Nilihamaki kuona wote wamepewa cocktail/
Walikunywa nakula bata walikunywa hata mziki waliruka mpaka mafundi walilewa pombe/

Wakasema huyu ni mjinga hajielewi/
Kisha wakanituhumu mim ni mlevi/
Wakati wamelewa wao...
Wakanipa matusi ya kienyeji/
Hawakutaka kusikiliza hata semi/

Nilimuona nahodha nikahisi nimeipata nafuu/
Alikuwa kando ya mrembo Fulani hivi daraja la juu/
Gauni refu mwili mzima amepakaza tattoo/
Aliponiona aliendelea kuikata tamboo/

Kweli starehe inaweza kukufanya hauoni/
Kukufanya hauoni...
Kwani licha ya kujua nipo hapo kutoa taarifa nahodha na mrembo waliendelea kushikana maungoni/

Nahodha akaipaza miguno/
Akinipuuza,, mrembo nae akafuata mkumbo/
Nahodha akachukua chupa akakata mafundo/
Wakaendelea kupapasana mifumo/
Ya viungo vyao vya uzazi/
Walikuwa radhi kuzika shift/
Hawakusikia chochote nilichosema..
Nakumbuka mrembo alidiriki kuniita mwizi/
Nikafuatwa nikaja kupigwa na walinzi/

Wenzangu waliogundua ubovu wa chombo walihofu/
Wakaamka wakawahi kubeba vyombo vya wokovu/
Walikaa kimya sababu tu ya ubinafsi mm nikabaki Ili niziokoe roho za wachovu/

Ilikuwa bahati mbaya hakuna aliesadiki/
Mshereshaji akaongeza sauti kubwa ya mziki/
Kiasi sauti yangu ikaanza kuwa haisikiki/
Walinzi walitumwa wanidhibiti/
Nilifungwa kwenye chumba chenye Giza chini nisihame/
Nikachapwa mijeledi 30 na minane/

Nikapambana nikatoroka na mtumbwi kwenda kando/
Usalama wangu ulianza hapo/
Nilishuhudia kila inchi ya Ile meli ikizama/
Roho za kila mkwezi zikihama/
Toka uhai kwenda KIFO/
Sikufurahi kuona hivyo/
Ila sikuwa na jambo ningeweza Fanya/
Wakati walokole wakiombea kupona/
Tajiri na masikini waligombea maboya/
Wanazi na walionicheka wakasema mim ni zuzu walikufa wote hata walionisema kinoma/

Ahadi ya maisha mapya ilisemwa/
Ila hakuna aliekumbuka/
Pesa zilizagaa na hazikuguswa/
Hata waumini walioitamani mbingu na kuisifu kumbe wote waliogopa kufa/
Waliokuwa wanajikweza na ukubwa na ubosi mwingi/
Waliishia majivuni/
NJIA walizibuni waliua mpaka wenza Ili kufosi kingi/
KIFO kiliwatia mbavuni/

Walikufa wengi kama kuku kote walizagaa/
Hata wanajeshi waliozijua kareti walidedi maana ujuzi wa mitutu haukufaa/
Mbele ya kufa..
Hakuna mwenye nguvu au shujaa/
Nilishuhudia makafiri wakiungama/
MASIKINI na matajiri waligusana/
Utu uliwatoka uhasi ulisogea/
Tofauti za kabila na rangi zilipotea/

Watu wenye bendi na t-shirt zao za kijani/
Walisahau kuwa nao pia wapo ndani/
Milango iliyokuwa wazi yote ilijifunga walipiga kelele na mwisho walikufa maji/
Washahiri waswahili na TASHTITI zao/
Matajiri na masikini wote chini yao/
Kwaya hazikutoa sauti ndimi zao/
Walikufa wote mpaka mahujaji na dini zao/

Wakati wa kufa hakuna dawa/
Hakuna kiongozi hakuna chawa/
Hakuna tofauti ya Mali na milki zetu kwenye kufa hata wenye nacho na wasokuwa nacho wanakuwa sawa/

Hazikusaidia diplomasia za digitali/
Asili ilihakikisha waliosalia hawafiki mbali/
Waliendelea kungoja msaada kwa tumaini mwisho wote walikufa sababu ya baridi Kali/
Walikufa makini..
Sababu ya wapuuzi wachache waliofanyia uzembe tangazo langu/
Wamiliki walikula bima wakasingizia ajali ilihali meli ilizama mbele ya macho yangu/

Viongozi hawakubebwa na vyeo vyao/
Maana wote walikuwa mbali na ridhaa/
Niliona kofia za ufalme zikielea kando yao/
Ila hakuna aliekuwa hai kuzivaa/
Niliwapa taarifa lakini wakanitwika maudhi/
Waliishia kulia na hazikusikika sauti/
Walipambana mwisho yaliwafika mauti/
Nilibaki hai kuziandika sarufi/

✍🏾✍🏾DIZASTA VINA✍🏾✍🏾
 
Back
Top