Kasomi
JT Founder
Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Reddit, mmoja wa waasisi wake, Steve Huffman, ametangazwa rasmi kuwa bilionea, hadhi iliyochelewa lakini iliyojaa mafundisho kwa kizazi cha wagunduzi.
Safari yao ilianza mwaka 2001, alipopatana na Alexis Ohanian chuoni. Wazo lao la kwanza halikufanikiwa, lakini ndipo Paul Graham, mwekezaji wa Y Combinator, alipoona kitu ndani yao. Aliwapa dola 12,000 na wazo moja tu:
"Kujenga Ukurasa wa Intaneti"
Wakiwa na matumaini na deni la kuaminiwa, walihamia Medford, Massachusetts. Ofisi yao ilikuwa meza mbili zilizounganishwa; pazia hawakuwa nayo, walitundika taulo dirishani. Wimbo uliokuwa ukisikilizwa muda mwingi? Hollaback Girl wa Gwen Stefani.
Baada ya wiki tatu tu, Reddit ikazaliwa.
Mwaka mmoja baadaye, waliuza sehemu kubwa ya kampuni kwa Condé Nast kwa makadirio ya dola milioni 10–20 wakati huo hatua iliyochukuliwa kama ya haraka kupita kiasi.
Lakini miaka 20 baadaye, hatua hiyo haionekani tena kama kosa. Reddit imekuja kuwa moja ya majukwaa makubwa duniani, na Steve Huffman sasa ni bilionea.
Ni ushahidi kwamba wakati mwingine, mafanikio makubwa huja polepole, lakini yakifika, yanathibitisha kila kusubiri kulikuwa na thamani.