Kasomi
JT Founder
Mwanzilishi wa tovuti maarufu ya NetNaija, Emmanuel Analike, ameendelea kushikiliwa gerezani baada ya ombi lake la dhamana kukataliwa na Mahakama Kuu ya Abuja.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Mkuu wa mahakama hiyo, Suleiman Liman, katika kesi inayomkabili Analike ya kumiliki, kunakili na kusambaza filamu, muziki pamoja na kazi nyingine za sanaa bila idhini ya wamiliki halali wa maudhui hayo.
Akiwa mahakamani, Analike alikana mashtaka yote yanayomkabili. Hata hivyo, Jaji Liman hakutoa uamuzi wa papo hapo kuhusu ombi lake la dhamana, badala yake aliahirisha kesi hiyo hadi Jumatatu, Machi 9, 2026.
NetNaija ni mojawapo ya tovuti maarufu barani Afrika, iliyopata umaarufu mkubwa kwa kuruhusu watumiaji kupakua filamu, muziki na tamthilia mbalimbali bila malipo. Umaarufu huo pia umeibua mijadala mikubwa kuhusu haki za umiliki wa kazi za sanaa (copyright) na matumizi ya maudhui mtandaoni.