Advertise here

Usiyoyajua kuhusu Mtandao wa Telegram

Kasomi

JT Founder
1487

Haya ni baadhi ya mambo ambayo wengi hawawezi kuyajua kuhusu Telegram:

1. Telegram haimilikiwi na kampuni kubwa ya biashara kama Meta
Telegram ilianzishwa na Pavel Durov, mwanzilishi wa VKontakte (VK), mtandao maarufu wa kijamii nchini Urusi. Ni kampuni binafsi isiyo na uhusiano na makampuni kama Facebook au Google.

2. Telegram haiko na ofisi rasmi ya kudumu
Waanzilishi wake walihamia kutoka nchi moja hadi nyingine kwa muda mrefu, wakidai kuwa wanakwepa udhibiti wa serikali. Telegram inaendeshwa kwa njia isiyo ya kawaida (decentralized team).

3. Inatumia mfumo wa Cloud-Based
Unapofuta app ya Telegram au kubadili simu, unaweza kurudisha kila kitu (picha, meseji, mafaili) kwa sababu data zako zinahifadhiwa mtandaoni.

4. Ujumbe wa Siri (Secret Chats)
Tofauti na meseji za kawaida, secret chats hazihifadhiwi kwenye server za Telegram. Zinapatikana tu kwenye vifaa vya waliotumiana ujumbe na zinaweza kujifuta zenyewe.

5. Telegram haina matangazo (ads) kwenye chats
Ingawa Pavel Durov alisema wanaweza kuanza kuweka matangazo kwenye public channels, chats binafsi bado hazina ads.

6. Telegram ina uwezo wa vikundi vyenye hadi wanachama 200,000
Huu ni uwezo mkubwa ukilinganishwa na WhatsApp.

7. Ni chanzo huria (Open API)
Watu wanaweza tengeneza bots, apps au tools kwa kutumia Telegram API bila malipo.

8. Inatumika sana kwenye maandamano na harakati
Kutokana na encryption na usalama wake, wanaharakati na waandamanaji wengi hutumia Telegram kuwasiliana bila kufuatiliwa.

9. Telegram haitumii data zako kwa matangazo
Tofauti na baadhi ya apps, Telegram haikusanyi taarifa zako kwa ajili ya kuuza kwa makampuni ya matangazo.

10. Ina desktop version isiyohitaji simu
Tofauti na WhatsApp Web, Telegram Desktop inaweza kufanya kazi bila kuwa na simu yako karibu.

11. Inaruhusu kutuma mafaili makubwa hadi 2GB (sasa hadi 4GB)
WhatsApp ni hadi MB 100 tu, lakini Telegram unaweza kutuma video, software, au mafaili makubwa kabisa bila shida.

12. Bots za ajabu ajabu
Kuna bots za kutafuta muziki, ku-download video za YouTube, kubadilisha lugha, kucheza games, au hata kujifunza somo moja kwa moja.

13. Uwezo wa kuhariri meseji hata baada ya kuituma
Kama ulituma typo au ulisema kitu vibaya, unaweza ku-edit badala ya kufuta.

14. channels na Supergroups zenye watu hadi 200,000+
Telegram ndio mtandao unaoweza kuunganisha idadi kubwa ya watu mahali pamoja nzuri kwa matangazo au jumuiya kubwa.

15. Themes na customization nyingi
Unaweza kubadilisha muonekano wa Telegram yako jinsi unavyotaka rangi, fonts, na zaidi.

16. Auto-download control kwa kila aina ya mtandao
Unaweza kudhibiti kama media ishuke kwenye Wi-Fi, data au roaming kwa uhuru kabisa.

17. Username sharing bila kutoa namba ya simu
Unampa mtu username, anaku-inbox bila kuhitaji namba yako ya simu.

18. Telegram Stories (feature mpya)
Kama Instagram na WhatsApp Status lakini Telegram stories zina settings zaidi za faragha na muda (unaweza set status ikae hata wiki moja au siku kadhaa).

19. Multi-account support
Unaweza kutumia akaunti zaidi ya moja kwenye app moja bila ku-log out.

20. Unaweza kutumia Telegram bila namba ya simu! (feature mpya)
Sasa unaweza kujiunga na Telegram kwa kutumia anonymous username kupitia blockchain-based number (Fragment) badala ya SIM card. Hii inamaanisha unaweza kuwa na Telegram account bila kutoa namba yako ya simu kabisa – kwa faragha ya hali ya juu.
 
Back
Top