john achila mukumwa
Member
Jinsi ya kumshinda shetani
Shetani ni nani?
Tafsiri ya jina shetani ni ‘mshitaki’ au ‘mchongezi’. Kazi yake ni kuwashitaki watakatifu mbele za Mungu. Jina lingine la shetani ni Lusifa, maana yake nyota ya alfajiri (Isaya 14:12).
Jina hili Lusifa aliitwa kabla hajaasi, baada ya kuasi ndipo akaitwa shetani.
Alikuwa ni malaika wa Sifa (Kerubi) huko mbinguni. Alikuwa ni mzuri kwa mwonekano, na mkamilifu katika njia zake zote. Aliishi katika taratibu za Mungu, na katika njia za Mungu. Hivyo, alipata heshima kubwa mbinguni zaidi ya malaika wengi (Ezekieli 28:14).
Alikuwa mkamilifu mpaka siku uovu ulipoonekana ndani yake (Ezekieli 28:15).
Kwa sababu ya uzuri wake, moyo wake ukainuka, akataka kujiinua, awe kama Mungu, aabudiwe kama Mungu, na kwa ujuzi wake mwingi, akashawishi theluthi moja (1/3) ya malaika mbinguni waambatane naye.
Vita, vikali vikatokea mbinguni kati ya malaika waliokataa kuungana na Lusifa na malaika waliokubali kuungana naye. Mwisho wa siku Lusifa pamoja na malaika wake walishindwa vita vile, na kutupwa chini duniani (Ufunuo 12:7).
Vita hiyo bado haijaisha. Vita ya kwanza ilipiganwa mbunguni, kati ya malaika walio upande wa shetani na wale walio upande wa Mungu. Malaika waliokuwepo upande wa Mungu wakashinda.
Lakini vita ya pili na ya mwisho, inapiganwa hapa duniani, na hata sasa bado inaendelea, na itaisha mwisho wa dunia.
Shetani anapigana vita usiku na mchana
Shetani anapigana vita na watiwa-mafuta walio duniani na “kondoo wengine” (Yoh 10:16). Lengo lake ni kuwameza watumishi na waumini wengi wa Yehova kadiri iwezekanavyo, na katika muda mfupi uliobaki (Ufunuo 12:9, 12):
9 "Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu".
Je, tunaweza kumshinda shetani?
Ndiyo! Kabisa! Biblia inasema: “Mpingeni Ibilisi, naye atawakimbia ninyi” (Yak 4:7).
Pia, “Chukueni msimamo mkampinge (shetani), mkiwa imara katika imani” (1Pet 5:9): "Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani".
TUNAWEZAJE KUEPUKA MITEGO YA SHETANI
1. WOKOVU
Wokovu hufanya kuwa na Kristo ndani yako. Hilo ndilo jambo la kwanza. Kamwe huwezi kumshinda shetani ikiwa upo nje ya Kristo.
Ndicho kilichowakuta wale wana wa Skewa, walipotaka kutoa pepo kwa jina la Yesu.
Lakini yule pepo akawaambia, Yesu namjua, na Paulo namfahamu, lakini je ninyi ni akina nani?
(Matendo 19: 13 Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. 14 Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. 15 Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? 16 Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile, hali wa uchi, na kujeruhiwa.
Wokovu, ni Kristo ndani yako, kwa hiyo, nguvu zote za adui huyeyuka mara moja. Mtu aliyempokea Yesu, shetani kamwe hamwezi, kwa sababu anamwona Kristo ndani yake.
2. WEKA NENO LA MUNGU NDANI, utamfukuza shetani
Kuweka Neno siyo, kukariri vifungu vingi vya biblia, hapana, bali ni kufahamu “ukweli” (ufunuo) wa kila Neno unaloliweka moyoni mwako na kulitekeleza. Pale jangwani, Yesu alipokutana na shetani, alimjaribu kwa Neno hilo hilo. Lakini Yesu akamwambia kweli yote ikoje.
Kitabu cha Mathayo 4 kinasema: 6 "akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako".
Ni muhimu kulifahamu Neno la Mungu katika kweli yake. Hiyo huchangiwa na kufundishwa kwa ufasaha Neno la Mungu na Walimu, kwa sababu Roho Mtakatifu atasema na wewe kupitia wao. Lakini pia kumpa Roho Mtakatifu nafasi ya moja kwa moja kukufundisha. Vinginevyo adui atakudanganya sana, hususan kupitia manabii wa uongo, kwa sababu hulijui Neno vema.
3. LITII NENO
Stahimili majaribu yake yote.
Kulifahamu Neno, na kuijua kweli, ni jambo muhimu, lakini bado shetani anaweza kupata mianya ya kukunasa, endapo hutaweza kulitii Neno.
Penda utakatifu, penda kutendea kazi kile unachofundishwa. Yesu alisema, wapo watu wasikiao tu, lakini wapo wasikiao na kuyatendea kazi. Wote hujaribiwa kwa pepo, mafuriko na mvua za shetani.
Yule aliyejijenga juu ya fundisho tu, na siyo kutendea kazi fundisho, ndiye huyo anayechukuliwa na mafuriko.
Mathayo 7 inasema: 26 "Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; 27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa".
Mateso mengine huwapata watu kwa sababu ya dhambi. Kuishi maisha matakatifu, humnyima adui mlango wa kukushambulia kwa namna yoyote. Ishi kwa kufuata na kutekeleza Neno.
4. MAOMBI
Huharibu mipango ya ibilisi.
Unaweza ukawa umeokoka, lakini shetani akapata nguvu za kukusumbua kwa majaribu, kwa sababu unashindwa kutimiza baadhi ya wajibu wako kama muamini. Yesu alisema katika Mathayo 26:41: "Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu".
Yesu, japokuwa alikuwa ni mkamilifu hana dhambi, alijaribiwa na adui, wewe ni nani usikutane na hayo? Usipokuwa mwombaji, uvivu ukakumeza, unaona shida kuomba kila siku, kuhudhuria mikesha, ujue tayari upo majaribuni. Hata kama utajiona upo sawa, fahamu tu hapo ulipo kuna eneo fulani adui anakusumbua, utakuja kugundua pindi utakapoanza kuwa mwombaji. Ndiyo maana MAISHA YA WOKOVU HAYATENGWI NA MAOMBI. Shetani akimwangalia mwombaji anaona moto mkali umemzunguka, hawezi kujiamulia tu kufanya analotaka kwake.
5. KUBALI KUWA MJINGA
Utamuweka shetani chini ya miguu yako.
Maandiko katika Warumi 16: 19 "Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya. 20 Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi".
Hapo anasema, tuwe wajinga katika mambo mabaya. Ni nafasi kubwa kwa Mungu kumweka shetani chini ya miguu yetu. Kwa mfano, unapokuwa hujui kuhusu mitindo mipya ya kidunia, siyo mfuatiliaji wa miziki ya kidunia, muvi mpya mpya zilizotoka duniani. Yaani kwa ufupi, unapitwa na mambo ya kidunia yasiyokuwa na maana kwako. Kinyume chake, unakuwa na ujuzi na hekima katika mambo ya rohoni, jua hapo umemshinda shetani kwa sehemu kubwa. Hapo shetani hana kitu kwako, kwa sababu bidhaa zake, huna mpango nazo, hununui chochote kwake. Wewe siyo mteja wake. Kuipenda dunia ni kuwa adui wa Mungu, na rafiki wa shetani.
6. HUBIRI NENO
Utamwangusha adui kutoka juu.
Watu wengi hudharau ushuhudiaji. Tunapokuwa na moyo mmoja wa kuitenda kazi ya Mungu, adui hawezi kukaa juu ya anga hili, kutupinga.
Tunalisoma wapi hilo? Utakumbuka wakati ule Bwana alipowatuma wanafunzi wake wawili wawili kuhubiri, waliporudi kwa furaha, huku wakimwambia Bwana hata mapepo yanawatii. Yesu akawaambia nalimwona shetani akianguka kutoka juu kama umeme. Kuonyesha kuwa kitendo cha wao kuhubiri, adui alikuwa anaporomoka kwa kasi sana.
Tazama Mathayo 10: 17 "Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. 18 Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme".
Kwa kuzingatia mambo hayo peke yake, utakuwa siyo tu umemdhibiti adui katika kila nyanja, bali pia umemshinda na kumteka.
Ni wajibu wetu kuboresha mahali ambapo hapako sawa, ili tuujenge ufalme wa Mungu na kuziangusha kazi za shetani.
Basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani, naye atawakimbia (Yakobo 4:7).