Advertise here

Kiongozi wa Korea Kaskazini Amchagua Binti yake kumrithi kiti cha Urais

Kasomi

JT Founder
KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI AMCHAGUA BINTI YAKE KUMRITHI KITI CHA URAIS
04nkorea-successor-mktj-articleLarge.jpg

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amemchagua Binti yake Kim Ju Ae kurithi nafasi yake ya Urais.

Uthibitisho huo unakuja baada Binti huyo kuonekana mara kwa mara kwenye hafla za Serikali, mara nyingi akiandamana na Baba yake katika hafla zinazoonekana kuwa za kisiasa.

Kim Ju Ae, anayeaminika kuwa na umri wa miaka 13, alionekana hadharani kwa mara ya mwisho mnamo 2022, alipoandamana na babake kukagua kombora la masafa marefu.

Tangu wakati huo, ameonekana mara kwa mara kwenye vyombo vya habari vya serikali, kwenye gwaride la kijeshi, na ziara za serikali, pamoja na safari ya hivi karibuni ya Beijing.

Wachambuzi wanasema mwonekano wake unatoa ujumbe mzito nchini Korea Kaskazini, ambapo uchunguzi wa picha na video wa maafisa wa serikali unadhibitiwa sana.

Wadadisi nchini Korea Kaskazini wanashangaa kwa nini mchakato wa kumrithi umeanza mapema, wakati Kim Jong Un bado ni mchanga na anaonekana kuwa na afya nzuri.

Kufikia sasa, wachambuzi wanasema Kim Ju Ae inaonyesha kwamba anaandaliwa kwa ajili ya jukumu la muda mrefu, ingawa hilo linaweza kubadilika kwani mustakabali wa Korea Kaskazini haujulikani.
 
Back
Top