Korea Kaskazini imekubali kurusha mechi za Ligi Kuu ya England lakini kwa masharti maalum

Kasomi

JT Founder
Korea Kaskazini imekubali kurusha mechi za Ligi Kuu ya England lakini kwa masharti maalum:
1740988996792.jpg

Matangazo Yatacheleweshwa kurushwa.
Mechi hazitaonyeshwa moja kwa moja (live); badala yake, zitacheleweshwa kwa miezi kadhaa na kufupishwa hadi dakika 60 badala ya dk 90

Kuondolewa kwa Wachezaji wa Korea Kusini:
Picha zinazoonyesha wachezaji wa Korea Kusini kama Son Heung-min (Tottenham), Kim Ji-soo (Brentford), na Hwang Hee-chan (Wolves) zitafutwa. Mechi zinazohusisha wachezaji hawa mara nyingi hazionyeshwi kabisa Korea Kaskazini.

Marekebisho ya Maandishi Uwanjani:
Maandishi ya Kiingereza yanayoonekana viwanjani yatafunikwa na picha za Kikorea ili kuweka maudhui kulingana na sera za nchi hiyo.

Kuondolewa kwa Alama za LGBTQ+ (Ushoga)
Matukio yanayoonyesha alama za LGBTQ+ yatahaririwa na kuondolewa ili kuendana na viwango vya utangazaji vya Korea Kaskazini.

Hatua hizi zinaonyesha jinsi Korea Kaskazini inavyodhibiti na kurekebisha maudhui ya kimataifa ili yaendane na sera zake za ndani na maadili ya kitamaduni.
 
Back
Top