Advertise here

Kiongozi wa chama cha People's Liberation – PLP nchini Kenya Martha Karua anasema amekataliwa kuingia Tanzania

Kasomi

JT Founder
Screenshot_20250518-114607~2.png

Kiongozi wa chama cha People’s Liberation – PLP nchini Kenya Martha Karua anasema amekataliwa kuingia Tanzania. Karua amesema kwenye mtandao wa X kuwa yeye, pamoja na wanaharakati wawili wa haki za binaadamu Gloria Kimani na Lynn Ngugi walizuiliwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili mapema leo Jumapili.

Wanaharakati hao watatu walikuwa Tanzania kwa mwaliko wa Jumuiya ya Wanasheria wa Afrika Mashariki.

Ziara yao inajiri wakati kesi inayomkabili kiongozi wa upinzani Tanzania Tundu Lissu inatarajiwa kusikilizwa Jumatatu katika mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam.
 
Back
Top