Kasomi
JT Founder
Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo amefariki dunia katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa za kifo chake zimetolewa usiku wa kuamkia leo ljumaa,
Februari 20, 2025 na Askofu Kuu wa Jimbo hilo, Yude Ruwai'chi.
“Kwa masikitiko makubwa leo tarehe 19/02/2026 saa 04:00 usiku huu mpendwa baba yetu Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, ameitwa nyumbani kwa Baba wa milele akiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam. wa Milele
Taarifa za mazishi zitawajia mara baada ya mipango
kukamilika. Tumwombee apumzike kwa amani.
Raha ya milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele
Umwangazie, Apumzike kwa Amani, Amina.,”