Kasomi
JT Founder
Fatma Karume kutoka Familia ya Viongozi hadi kuwa Mwanaharakati
Huyu ni mwanaharakati kutoka katika familia ya viongozi; babu yake Shekhe Abeid Karume alikuwa muasisi na Rais wa kwanza wa Zanzibar, baba yake Aman Abeid Karume alikuwa rais wa awamu ya saba wa visiwa hivyo huku baba yake mdogo Ally Abeid Karume amewahi kuwa balozi na waziri katika awamu za serikali mbalimbali.
Fatma maarufu kama Shangazi kitaaluma ni mwanasheria aliyezaliwa Juni 15, 1969, na amekuwa mwanaharakati wa muda mrefu akitumia taaluma yake ya sheria katika kufanya shughuli zake za uanaharakati.
Baada ya kumaliza elimu ya sekondari alianza kusoma sheria huko Strasbourg, Ufaransa hadi 1991. Mwaka 1992 akaendelea kupata shahada ya awali ya sheria kwenye Chuo Kikuu cha Sussex.
Kukuliwa kwenye familia ya viongozi au kuwa mtoto wa rais mstaafu na mjukuu wa muasisi wa taifa hilo, pengine kungemfanya kuunga mkono masuala mengi yanayofanywa na serikali inayoongozwa na chama cha mapinduzi (CCM), ambacho wazazi wake wamekuwa wanachama kwa muda mrefu, lakini imekuwa tofauti.
Amekuwa mkosoaji mkubwa wa hatua nyingi zilizofanywa na zinazofanywa na utawala wa chama hicho, na kujikuta kwenye dhahma za mara kwa mara na mamlaka.
Ofisi yake ilipigwa bomu ikiwa ni moja ya mashambulio dhidi yake. Alifukuzwa katika Kampuni ya Uanasheria ya IMMMA Advocates aliyoshiriki kuianzisha.
Akieleza kufukuzwa kwake, anahusisha na harakati zake.
"Hii ni kuwajulisha nyote kwamba, nimefukuzwa kwenye ofisi niliyoijenga. Uovu wangu, uanaharakati," aliandika Fatma kwenye ukurasa wake wa twitter Septemba 21 mwaka 2020.
Aliwahi kuwa rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019 Aliondolewa pia uraisi wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) kabla ya kufutwa kabisa kwenye orodha ya mawakili ili asiweze kufanya kazi za uwakili nchini hasa bara kulikotolewa hukumu hiyo. Lakini hii haijamzuia Fatma kuendelea na msimamo wake na harakati zake.