Kasomi
JT Founder
MTANZANIA WA KWANZA KUPATA SHAHADA YA UZAMIVU (PhD) KUTOKA CHUO KIKUU MAARUFU DUNIANI CHA HARVARD
Pichani ni Justinian Rweyemamu ndiye Mtanzania wa kwanza kupata Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu maarufu duniani cha Harvard.
Justinian Rweyemamu alikuwa bingwa wa hesabu, uchumi na philosophy ( falsafa ), ni mzawa wa kijiji cha Katoma huko mkoani Kagera ambapo alizaliwa mwaka 1942.
Justinian aliibuliwa na taasisi iitwayo Rockefeller ambayo ilitambua uwezo mkubwa sana na wakustaajabisha aliokuwa nao.
Uwezo wake wa kustaajabisha ulipelekea mpaka maprofessor wabobevu wa chuo cha Harvard kupigwa na butwaa kutokana uwezo uliopitiliza alizokuwa nao Justinian, alikuwa kijana mdogo sana aliyeibua gumzo na kutingisha chuo kizima cha Harvard.
Taarifa zake zikamfikia mwalimu Nyerere akamwomba arudi nchini wasaidie kuijenga nchi kwa sababu ujuzi wake ulihitajika Sana kwa kipindi hicho, bila hiyana alikuja na akawa mkuu wa idara ya uchumi pale Chuo kikuu cha Dar es salam akiwa na umri mdogo Sana miaka 28, pamoja na umri wake kuwa mdogo aliweza ongoza vyema kitengo chake na kutoa michango mikubwa Sana.
Tofauti ilikuja kutokea kwenye Itikadi na mitazamo ya kwendesha uchumi wa nchi, yeye alikua akiamini kwenye utikadi za kibepari huku Mwalimu akiamini katika falsafa za wakina Karl Marx waasisi wa itikadi za kisoshalist. Hapo tukapoteza kichwa cha hatari Sana kilichokuwa kimejaa madini mengi sana na yenye thamani zaidi ya Tanzanite.
Inasemekana baada ya kutofautiana na mwalimu alirudi nchini Marekani (mwenye uhakika anaweza kuthibitisha).
Justinian Rweyemamu alifariki dunia mwaka 1982.