Google Maps OSINT

Raven

New member
Google Maps OSINT
3b9785234a0c54c34b39dcea0c0e624c.jpg


Google Maps ni app inayomsaidia mtu kujua yupo sehemu gani duniani kwa msaada wa teknolojia ya GPS ambayo sensor yake huwa ipo ndani ya kifaa chake cha ki-electronic (simu, computer, tablet au gari)

Google Maps inasaidia pia kufahamu directions ikiwa unataka kwenda sehemu fulani. Inasaidia kufahamu sehemu mbalimbali kama hotel, shule, vituo vya kujaza mafuta, makanisa, maduka, mitaa n.k

Leo takufundisha namna ya ku-search ukiwa Google Maps.

1. Ku-search kwa kutumia jina.
Hapa utaandika jina la sehemu unayotafuta. Kama nii hotel basi utaandika jina la hotel.

2. Ku-search kwa category
Category ni kama kundi la vitu au sehemu zinazotoka jamii moja mfano guest houses, hotels, oil stations, schools n.k. ikiwa unatafuta shule za msingi karibu na eneo ulilopo unaweza andika hivi: Primary schools near me.

3. Ku-search sehemu karibu nawe. (Near me)
Mfano ulikuwa safari ya kwenda Mbeya baada ya kufika Mbeya ukawa unataka kwenda kulala hotelini unaweza search Hotels near me, utapewa list ya kuchagua hotels zilizo karibu nawe.
4. Ku-search eneo maalumu. (In)
Mfano unataka kujua vyuo vilivyopo mkoa wa mwanza na Ungependa kufanya application baada ya researching. Unaweza andika kama hivi: colleges in Mwanza.

5.Ku-search kwa kutumia jina la huduma.
Mfano huduma ya car wash - car wash. Huduma ya pharmacy - pharmacy. Huduma ya parking - parking n.k

Google Maps inatumika kwenye mambo mengi ila upande wa OSINT inaweza kukusaidis kupata taarifa za eneo fulani, business informations, business reviews, kuona picha za maeneo husika kutoka kwa watumiaji wengine, kujua mazingira ya eneo fulani, Geo codes, njia za kupitia (navigation) etc etc.
 
Back
Top