Kasomi
JT Founder
Idara ya Sheria ya Marekani (DoJ) imependekeza kwamba Google iuze browser yake ya Chrome na kuwekewa vikwazo kwenye mfumo wa Android kama sehemu ya mpango wa kuivunja na kuipunguza nguvu kampuni ya Google/Alphabet.
Uamuzi huu unakuja baada ya jaji wa shirikisho kuamua kuwa Google ni kampuni ya ukiritimba katika data za watumiaji, ikitumia nguvu zake kutoza bei za juu kwa matangazo kwenye platform zake.
Hata hivyo, Google inapinga pendekezo hili, ikidai kuwa litawaumiza watumiaji na kuathiri uongozi wa teknolojia wa Marekani.
Shtaka hili lilifunguliwa awali mwaka 2020, likidai kuwa Google ililipa mabilioni kwa watengenezaji wa vifaa ili kuhakikisha Google Searcg yake ya utafutaji inakuwa chaguo-msingi. Google inalipa Apple na Samsung, ili ziweke Google Search kuwa default search engine kwenye vifaa vya Apple na Samsung.
Pendekezo la kuivunja kampuni linaweza kuwa na athari kubwa kwa mtindo wa biashara ya Google, likiathiri zaidi ya 60% ya biashara.
Hatma ya hali hii bado haijulikani, huku kukiwa na kesi nyingi za mahakama na rufaa zinazotarajiwa.