Kasomi
JT Founder
GOOGLE YAMUOMBA TRUMP KUBATILI AGIZO LA KUUZA CHROME
Google inafanya juhudi za mwisho kuzuia hatua ya kulazimishwa kuuza kivinjari chake maarufu, Google Chrome. Kampuni hiyo imeiomba serikali ya Trump kubatilisha agizo hilo lililotolewa chini ya utawala wa Biden, ikidai kuwa linaweza kuhatarisha biashara yake na hata usalama wa taifa.
Kwa nini Google inapinga uamuzi huu? Serikali inadai kuwa kampuni hiyo inaendesha ukiritimba kwenye sekta ya utafutaji mtandaoni, lakini Google inasisitiza kuwa Chrome ni sehemu muhimu ya mifumo yake na kuiuza kutaleta madhara makubwa kwa sekta nzima ya teknolojia.
Je, Trump atasikiliza ombi la Google au ataendeleza msimamo wa Biden? Hili ni sakata kubwa linaloweza kubadili mustakabali wa kivinjari cha Chrome na biashara ya Google kwa ujumla.