Kasomi
JT Founder
Wakati wanaanga wanne wa misheni ya Artemis II wakiwa njiani katika safari ya siku nne kurejea duniani baada ya kusafiri umbali wa kihistoria wa zaidi ya kilomita 406,000 kuzunguka mwezi, mjadala kuhusu anga na uchunguzi wake umeibuka upya. Lakini mbali na sayansi na safari hii ya kipekee, kuna simulizi ya kushangaza inayozua swali, je ni nani anamiliki Mmwezi?Dennis Hope alipata wazo la kuuza ardhi kwenye mwezi baada ya talaka yake.
Jaribu kufikiria, umetoka kuachana na mpenzi wako, hauna pesa, halafu unapata wazo la ajabu kwamba "Nitauza mwezi na kujipatia kipato"
Najua inakaa wazo ambalo ni la kipekee
Lakini Dennis Hope, raia wa Marekani, alipata motisha ya kuuza mwezi. Alitajirika na kuwa milionea baada ya kuuza vipande vya ardhi kwenye mwezi miaka ya 1980.