Advertise here

Selection za kidato cha kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi zatoka 2026 Wanafunzi 246,197 wamechaguliwa

Kasomi

JT Founder
1000717001.jpg

Wanafunzi 246,197 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi kati ya hao wasichana 114,102 na wavulana ni 132,095 ikijumuisha wanafunzi 631 ni wenye mahitaji maalum.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, ameyasema hayo, leo, Juni 01, 2026 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari.

Wanafunzi 172,114 sawa na asilimia 69.9 wamechaguliwa kujiungana na kidato cha tano katika shule za Sekondari za Serikali. Wanafunzi hao wamechaguliwa kutoka shule 856 kati yahizo shule 825 ni za bweni na 25 ni za kutwa.

Wanafunzi 74,083 sawa na asilimia 30.1 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi kati.

Bonyeza hapa kuona selection hizo
 
Back
Top