Advertise here

New Alert: NECTA imetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026

Kasomi

JT Founder
NECTA imetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2026
1000778052.jpg

Baraza la Mitihani la Tanzania leo tarehe 6/7/2026 limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) na Mitihani ya Ualimu iliyofanyika Mwezi Mei, 2026.

Matokeo hayo yanapatikana kwenye tovuti ya NECTA

Bonyeza Hapa kutazama matokeo

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limefuta matokeo ya watahiniwa 58 baada ya kubainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani. Waliofutiwa matokeo ni watahiniwa 44 wa Mtihani wa Kidato cha Sita na 14 wa Mtihani wa Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi (DPEE), baadhi wakitajwa kutumia AI (Chatgpt).

Aidha, Baraza limekifungia kituo cha mitihani cha P5584 Excellency Open School kilichopo mkoani Manyara kutokana na kukiuka miongozo ya uendeshaji wa Mitihani ya Taifa. Kituo hicho kitaendelea kufungwa hadi NECTA itakapojiridhisha kuwa kinafaa kuendesha mitihani kwa usalama.
 
Back
Top