Advertise here

Rais Samia Mgeni Rasmi wa Tanzainia Comedy Awards (TCA)

Kasomi

JT Founder
Tanzania Comedy Awards imepata baraka za Mheshimiwa Rais samia suluhu kuhudhuria kama Mgeni Rasmi!
1740075007846.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi wa tuzo za wachekeshaji Tanzania 'Tanzania Comedy Awards' siku ya February 22,2025 ukumbi wa The Super Dome Masaki Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo #MwanaFA katika tukio la All-Star Comedy Festival, lilofanyika Mlimani City.

Baadhi ya mastaa wa uchekeshaji waliotokea All Star Comedy Festival ni Coy Mzungu, Leonardo, Ndaro, Shafii Brand,SaidSaid, Kipotoshi, Nanga OG, Masantula na Eliud.


Pia Mwanzilishi wa Cheka Tu alitoa neno akisema

"Kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika, Rais wa nchi anazindua tuzo za vichekesho—hatua kubwa kwa sanaa na wasanii wa Tanzania!

Kama Coy Mzungu, nimefurahi sana kwa sababu hii inaenda kuondoa mzigo wa kutafuta imani kutoka kwa wadau na wafadhili. Sasa, kila mmoja ataelewa kuwa hii ni tasnia inayojitegemea, yenye thamani kubwa ya kibiashara, na inayostahili kushirikiana na makampuni makubwa.

Wachekeshaji wenzangu, hii ni zaidi ya kubwa kwetu! Nimepokea simu nyingi kutoka nchi jirani wakitupongeza kwa hatua hii kubwa, siyo tu kwa Tanzania bali kwa Afrika nzima. Hii ni historia tunaiandika pamoja!

Pongezi kubwa kwa waandaji wa Tanzania Comedy Awards kwa juhudi kubwa kuhakikisha ndoto hii inatimia. Tupo nyuma yenu kwa hali na mali! Vichekesho vina thamani, na sasa dunia inashuhudia!"
 

Similar threads

Back
Top