Advertise here

Serikali imetangaza rasmi nafasi 41,500 za ajira katika sekta mbalimbali za umma

Kasomi

JT Founder
Screenshot_20251012-004833~2.jpg

Serikali imetangaza rasmi nafasi 41,500 za ajira katika sekta mbalimbali za umma ikiwa ni juhudi za kukabiliana na upungufu wa watumishi nchini. Nafasi hizo zitatolewa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na 2025/2026, huku mchakato mzima wa ajira ukitakiwa kukamilika ifikapo Novemba 2025.

Akitangaza ajira hizo kupitia vyombo vya habari jijini Dodoma 2025, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma Mkomi, amesema ajira hizo ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kada zitakazopatiwa ajira ni pamoja na elimu (nafasi 12,176), afya katika ngazi ya serikali za mitaa (nafasi 10,280), kilimo (nafasi 470), mifugo (nafasi 312), uvuvi (nafasi 47), na vyombo vya ulinzi vikiwemo Polisi, Magereza, Zimamoto na Uhamiaji (nafasi 7,000).

Mkomi ameelekeza Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kuhakikisha mchakato wa ajira hizo unakamilika kwa wakati, sambamba na kukamilisha mchakato wa nafasi 45,000 za ajira ambazo hazikujazwa katika mwaka wa fedha 2024/2025.

Amesema serikali inazitaka mamlaka zote zenye uwezo wa kuajiri kuhakikisha zinashirikiana kikamilifu katika kujaza nafasi hizo haraka ili huduma kwa wananchi zisiathirike kutokana na uhaba wa watumishi.
 

Similar threads

Back
Top