Advertise here

Je, Wajua kuhusu Artificial Intelligence (AI), Machine Learning na Robot?

Kasomi

JT Founder
Je, Wajua kuhusu Artificial Intelligence (AI), Machine Learning na Robot?

AI ni nini?

AI (Artificial Intelligence) ni akili au utashi bandia yaani uliobuniwa.

Tofauti ya AI na Robot:

Kwa kawaida robot ni kifaa au chombo au hata software ambayo inatumia teknolojia ya AI ili kufanikisha utendaji. Kwahiyo AI ni teknolojia yenyewe, hata hivyo maneno haya kuna muda unaweza kutumia kwa kazi moja. Hasa watengeneza magemu hutumia neno AI or roboti kama opponent (mpinzani) wa binadamu.

Wapi AI inatumika?

Hutumika katika viwanda na sehemu za ukaguzi kupitia robots na kompyuta. Hutumika katika mitandao kwa ajili ya auto-suggestion, ad-promotion, intelligent search nk.

Pia katika gaming mfano magemu ya mpira kama PES, FIFA nk. Pia katika magemu ya mashindano ya mbio (racing) kama Need for Speed, MotoGp nk.

Halikadhalika katika board games kama drafti, chess, othello nk.

Teknolojia gani AI hutumia?

Ni nyingi mno, Ila kwa upande wa board games maarufu ni MiniMax algorithms, NegaScout / NegaMax, AlphaBeta pruning na Machine Learning ambayo ndani yake ina vitu vingi kama NNUE (Efficiently updatable neural networks). Kwa kawaida teknolojia zaidi ya moja huweza kutumika ili kuifanya AI iwe na uwezo mkubwa.

Wengine pia hutumia opening na "end games database" kwa mchezo kama wa drafti ambapo kunakuwa michezo tofauti tofauti kama zaidi ya million moja inakuwa imerekodiwa then inakuwa highly compressed. Kila binadamu akicheza kete AI inaangalia katika Database ni mchezo gani unafuata kulingana na kete aliyocheza. But mfumo huu unahitaji analysis ya muda mrefu.

Shida inakuja kuna baadhi ya teknolojia zinachagua hardware mfano katika PC yenye CPU dhaifu AI haifanyi vizuri, na hii hasa kwenye Machine Learning na deep search algorithms. Topic kuu ya kutengeneza AI kwa ajili ya games hasa board games inaitwa "Game Theory" kwa anayetaka kuifuatilia. Of course hailipi kwa hapa Tanzania ila ni mapendeleo tu kuifuatilia, ni special kwa watu wanaopenda research za kuumiza kichwa.

Naamini mitandaoni yapo material ya kutosha kuhusu game theory. Java programming language imetumika kuanzia kwenye AI hadi GUI (graphical user interface).

Itaendelea
 

Similar threads

Back
Top