Fahamu kuhusu OSINT (Open Source Intelligence)

Kasomi

JT Founder
Anaandika @Raven

OSINT ni nini?​

Screenshot_20250617-182557~2.png

OSINT ni kifupi cha OPEN SOURCE INTELLIGENCE.

OPEN SOURCE - Chanzo cha wazi
INTELLIGENCE - Taarifa

Katika lugha ya kiswahili tunaweza sema OSINT ni Taarifa unazoweza kuzipata kutoka katika vyanzo wazi kuhusu jambo fulani kwa lengo fulani.

Kufanya OSINT = Kutafuta taarifa kwa lengo fulani.

TURUDI NYUMA KIDOGO STONE AGE KABLA YA INTERNET

Sasa bwana kule nyuma kupata information muhimu kuhusu issue zako hata umbea haikuwa cheap unaambiwa ni expensive.

Ukitaka info ili kujifunza namna ya kupika pilau au biriani katika kipindi hiki cha Informatzijua..
...Ila huko zamani ilikuwa tofauti kidogo naam, ukitaka info fulani sharti ufunge safari uzifate kwenye source iwe mtu au maktaba.

Kwenye swala la pilau unamtafuta chef mpishi unatoa hela anakuelekeza huku unachukua notes ukitaka practical sessions unalipia sema mababu zetu walikuwa wanapiga madusko kwa kuuza info tu..

Unaambiwa yule mtu wa shoe shine alikuwa anawapigisha story wateja wake huku anawauliza maswali kimkakati lengo tu apate taarifa/umbea kama Mange Kimambi hafu ukimuuliza swali hajibu utoa cash anafungua mdomo anakuuzia info.

Kwa hiyo hata kwenye mishe za ujasusi kusafiri safiri mpaka location kuspy na kukusanya info ilikuwa gharama.

Kiujumla vyanzo vya taarifa vilikuwa ni vichache ukilinganisha na sasa hata kwenye kupata material ya kujifunzia haikuwa rahisi

Hivyo baada ya kuja kwa internet vyanzo vya taarifa viliongezeka na kufanya taarifa ziwe rahisi kupatikana maana Ziko waziwazi yaani OPEN.

Hivyo wakaona hamna haja tena ya kutegemea sana njia za zamani za kupata taarifa labda kufanya udhibitisho wakaamua kudili na hivi vyanzo vipya vya taarifa vya waziwazi yaani OPEN SOURCE INTELLIGENCE.

Ladies and Gentlemen inasemakana OSINT ndio ilazaliwa.

Vyanzo vya wazi vyaweza kuwa
1. Mitandao ya Kijamii
2. Machapisho ya Blogi na Foramu
3. Tovuti za Serikali
4. Vyombo vya Habari
5. Tovuti za Utafiti wa Umma
6. Mashirika ya Kimataifa
7. Tovuti za Maktaba
8. Tovuti za Biashara na Viwanda
9. Tovuti za Teknolojia
10. Vitabu, majarida, magazeti...

Lengo Kuu la kufanya OSINT ni kutafuta taarifa kwa matumizi mbalimbali ambayo hutofautiana kati ya mtu na mtu.

Taarifa zitakazopatika kutokana kufanya OSINT zinaweza kutumika kusadia katika
- Kufanya utafiti kuhusu jambo fulani.
- kufuatilia mienendo ya watu mitandaoni (serikali).
- Kufanya upelelezi binafsi/mtu/shirika.
- Kurahisisha jambo fulani mf. Pentesting, Planning.
- Kujua location ya eneo fulani.
- Kufahamu taarifa za kipindi cha nyuma kuhusu mtu, eneo fulani.
- Kuthibitisha taarifa...

OSINT Tools.
Hizi ni zana ambazo husaidia pale unapokuwa unafanya OSINT ili kupata taarifa unazitafuta.
Tools hizi zipo nyingi na kila tool na kazi yake ila Baadhi ni
- Critical Thinking kufikiri kwa kina, kufanya observation na reasoning.
- Google Dorking
- Image Reverse Search.
- Face recognition.
- Metadata Extractors
- Social media OSINT.

Tuongee Tools

Critical Thinking hii inahusisha matumizi ya akili kwanza kuchambua ili kupata taarifa nusu nusu (Data) kabla ya kwenda kutumia tool zingine.

Hii inasaidia kurahisisha zoezi zima la OSINT maana itakupa sehemu ya kuanzia.

Hii critical Thinking nadhani inahitaji uwe ujuzi wa mambo mbalimbali kwenye knowledge base yako ambao utakusaidia kwenye ung'amuaji wa taarifa.

Google Dorking

Google Dorks

Kila mtu anaweza kusearch Google ili kutafuta taarifa, lakini sio kila mtu anajua kusearch Google na kupata taarifa anazozihitaji kwa 100%

Sasa kuna kitu kinaitwa Google Dorks. Google dorks ni mbinu za utafutaji wa taarifa pale unapokuwa unasearch Google.

Iwe unasearch taarifa kuhusu tukio fulani, articles, mtu, files etc kujifunza namna ya kusearch i.e Google dorks ni kitu muhimu sana maana hupunguza tabu wakati wa kufanya upekuzi.

Itaendelea....

Credit: Raven
 
Tuendelee sasa...

MBINU ZA KUTAFUTA DOCUMENT/ARTICLE/VUTABU/FILES PALE GOOGLE SEARCH.

Double Quote ""

Kupata matokeo sawasawa na kile unachotafuta weka maneno yako ndani ya double quote ""

Mf. "Mabala the farmer"
"48 Laws of power"

filetype:

Hii ni mbinu nyingine ambayo hutumika kutafuta file kwa kuandika jina la file na aina ya file
Aina za file ni kama docx,pdf, ppt, exe, jpg, svg e.t.c

Namna ya kusearch
Mf. filetype pdf The 50th Law

Hapa utaletewa kitabu cha The 50th Law katika mfumo wa pdf, tupo pamoja?.

Vitabu published recently huwa ngumu kupatikana maana watu wachache huwa navyo hafu wanaviuza na huwa sio popular sana hivyo kukipata mtandaoni bure inakuwa changamoto.

Kuna online community za vitabu, hivyo kama kitabu unachotafuta wanacho hafu na wewe ni member wanaweza kukubless.

Pia kuna watu huwa wanakusanya mavitabu kisha kuyaweka kwenye database na kuvihifadhi humo kisha kuunda website ambazo huwa na search engine zao ambazo Unaweza kuzitumia kutafuta kitabu unachohitaji na kukipakua.

Bado kuna Torrent sites tena huku watu hushare vitu vingi

Websites


Kuna hii online database kubwa ya vitabu/Library humu kuna vitabu vingi sana pamoja na documents mbalimbali. Unaweza tafuta kwa tumia jina la kitabu au La mwandishi. TUMIA LA MWANDISHI


Hii ni moja kati ya site za torrents humu tafuta kitu chochote tu hata movie ya 4k utapata tumia App ya Ku-Download torrents kama uTorrent App


Hii hapa site nyingine ya vitabu zamani ilikuwa inafanya kazi baadae ikawa inazingua kushusha mzigo sijui wahuni waliiloga anyway leo nimejaribu kushusha kitabu, kitabu kimeshuka inaonekana sahivi ipo sawa

Site: unachotafuta

Hii mbinu tunatumia kusearch ndani ya site husika kutoka Google search engine moja kwa moja kwenye site

Kwenye site unaweka site name hafu jina la kitabu/kitu

Mf. pdfdrive: Art of war sana kuanzia picha, video, movies, vitabu, games, courses, documentary hadi conn.... yaani mwendo wa kujipakulia minyama tu.

Face Recognition

Hii ni Technology ambayo hutumika kutambua sura ya mtu kwa kulinganisha na picha zenye sura za watu zilizopo kwenye database.

Picha hizi zinaweza kuwa zimechukuliwa kutoka kwenye mitandao ya kijamii na kuhifadhiwa kwenye database za kampuni yenye software.

Si mshawahi kusikia kuwa baya makampuni ya tech yanauziana dstay mara wawauzie CIA. Hata kwenye wakitaka info za mtu wanaingia kwenye software zao za Face Recognition wanaweka picha ya mtu hafu unaona inaanza kuscan then baadae inaleta matokeo na info zingine zinazohusiana na mtu husika.

Sasa bwana kuna hizi Face recognition tools ambazo unaweza kuzitumia wakati wa OSINT kama unatafuta info kuhusu mtu fulani.

Zipo za bure na kulipia, ninazozijua ni

FacechekID
www.facecheck.id

PimEyes


Hizo tools kutumia ni rahisi sana unachofanya ni kuweka picha (hakikisha sura inaonekana vizuri) then unabonyeza button ya search ikimaliza kuscan utaletewa picha zinazofanana sura n hiyo uliyoweka.

Ila majibu yanategemea na picha ya mtu unayemtafuta kama.

Ni mtu wa mitandaoni nikimaanisha anajipost post sana hii inakuwa rahisi kama sio ni ngumu kidogo nikimaanisha Unaweza usipate matokeo ya kurithisha.

Sura yake

Kama sio unique kidogo unaweza pata sura ya mtu mwingine wa kufanana nae mfano wachina na wakorea hawa ni pasua kichwa maana wanafanana sana.

IMAGE REVERSE SEARCH.

Hii ni tech nyingine ambayo husaidia kutafuta vitu vilivyomo kwenye picha kwa kutumia picha.

Mfano uneona gari hujui ni gari aina gani unaingia Google unasearch kwa kutumia picha (Google Lens) baadae sasa ndio unapewa mapicha picha mengi ya magari sawa na hilo la kwenye picha ukichagua moja unakutana info za kutosha.

Searching by image ndio hujulikana pia kama Image Reverse Search.

Are we together?

Image Reverse Search tools unaweza kuzipata kwenye App ya

Google Lens.
Pinterest.
Alibaba.

Kama simu yako haisapoti Google Lens App kama hii yangu kuna website huwa natumia imeunganishwa na Google Lens unaweza tumia pia.


FacechekID na PimEyes pia zinatumia Image Reverse Search lakini zenye zinazingatia uso tu.

Online Maps tools.

Hizi zinakupa taarifa kuhusu eneo unalolichunguza

Mfano tuseme mkoa wa Mwanza

Inapatikana wapi?
Mikoa jirani ni ipi?
Hali ya kijiografia ikoje?
Vyanzo vya maji?
Shughuli za kiuchumi.
Etc

Maps zingine ukiachana na Google Maps unaweza ziona kwenye picha.

Makundi ya watu ambayo hutumia pia OSINT kwenye mambo yao.
- Watu wa kawaida.
- Watafiti.
- Mashirika ya kijasusi
- Wapekupeku.
- Makampuni ya biashara

Hii list inaendelea... Unaweza Google kujua watu wengine zaidi.

End

Credit: @Raven
 
Back
Top