Advertise here

Yanayojiri mkutano mkuu maalum wa CCM. Kinana apita kwa kura zote 1,875 zilizopigwa

Kasomi

JT Founder
Leo ni mkutano mkuu maalum wa chama cha mapinduzi ambao pia utaenda kupitisha mabadiliko ya katiba ya CCM. Kwasasa anaongea katibu mstaafu wa CCM, Yusuph Makamba ambae anasema mchungaji Gwajima alimuuliza yeye kama mtabiri, anatabiri nini kwenye utawala wa mama Samia baada ya kutabiri ubatizo wa maji kwa Jakaya na ubatizo wa moto kwa Magufuli.

Makamba: Nikasema natabiri ubatizo wa maji na faraja, akaniuliza Gwajima, kwanini faraja? Nikamwambia bwana Yesu alisema bado kitambo kidogo mnaniona na bado kitambo kidogo hamnioni, wanafunzi walipofadhaika akawaambia msifadhaike nakwenda kwa baba yangu kuwaandalia makao lakini baba yango atawaletea mfariji mwingine.

Sasa kama Magufuli ameondoka, anaekuja si Rais tu, ni mfariji, sasa unatufariji maana maji tunapata, umeme tunapata, watoto wanasoma, mikopo ipo. Nikamuuliza Gwajima, basi akasema ungekuwa mchungaji wa kanisa langu, nikamwambia sitaki mimi muislam.

Kwahiyo mama usikasirike tunaposema tumekutabiria ubatizo wa maji na faraja na ilimradi watanzania wote wanafarijika, Rais ni wewe.

Pia Makamba ameongelea mgombea Urais 2025 ambae amesema ni mama Samia na amewaambia upinzani mgombea ni Samia na kama kuna anaejiandaa akae tayari.

Makamba anaendelea kwa kueleza alipotoka na Kinana na anamuelezea kama mtu aliyefanya nae kazi Korogwe ikiwa ni kazi yake ya kwanza akimtaja kama mtu mzuri na anaeweza kujishusha.

Mwisho Makamba anaisifu halmashauri kuu kwa kutambua uhodari wa Kinana na kutimiza ombi la Jakaya kwa kuomba wamtafutie kitu Kinana wampe, wenyewe wakaamua kumpa umakamu badala ya jengo na daraja.

Makamba: Sasa mheshimiwa Kinana tuna ligi 2025, tunataka kushika madaraka nchii hii hakuna kumuachia mtu mwingine, sisi tu.

Wewe sasa kocha msaidizi, sio wa Yanga wala sio wa Simba, ni kocha msaidizi wa CCM, msaidie mwenyekiti tushinde na wala na wewe usiogope.

=======

Kinachoendelea kwasasa ni zoezi la upigaji kura kwa makamu mwenyekiti aliyependekezwa, AbdulRahman Kinana.

12:46 pm; Spika wa Bunge anasoma taarifa ya uchaguzi

Idadi ya wajumbe waliopiga kura 1875

Kura halali 1875

Kura za hapana 0

 

Similar threads

Back
Top