Advertise here

Mwalimu Mkuu Gibson Mkomi Afanya Harambee Ujenzi wa Hostel Bugalama Geita

Kasomi

JT Founder
Screenshot_20251014-162516~2.jpg

Imeelezwa kuwa wanafunzi wengi wa kike wanakatisha masomo kila mwaka kutokana na umbali mrefu wa kuifata elimu katika kata ya Bugalama halamashauri ya wilaya ya Geita.

Gibson Mkomi Mkuu wa shule ya sekondari ya Bugalama ameamua kufanya harambee ya uchangiaji wa jengo la hostel kwa ajili ya watoto wa kike ambapo wamekuwa wakikutana na vishawishi vya mara kwa mara na hatimae kukatisha masomo.

Shule ya sekondari Bugalama ipo katika kata inayoundwa na vijiji vinne ambayo vipo mbalimbali hivyo kuepelekea wanafunzi kutembea umbali mrefu kufika shuleni na hatimae wengine kukata tamaa kumaliza masomo.

Kadhia hii imewagusa wanafunzi waliowahi kuhitimu katika shule ya sekondari Bugalama miaka ya nyuma kuchangia vitanda kwa ajili ya kuwahamasisha wadau wengine waweze kuguswa na harambee hii ya uhenzi wa hostel kwa ajili ya watoto wa kike

Wazazi na walezi wameushukuru uongozi wa shule kwa kuanzisha harambee hii jema kwa ajili ya mustakabari wa elimu ya watoto wao.
 

Similar threads

Back
Top