Mwigulu Nchemba ateuliwa kuwa Waziri Mkuu

Kasomi

JT Founder
1763017256060.jpg

Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteuwa aliyekuwa Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.

Mapema ya leo Novemba 13.2025 Mpambe (ADC) wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameleta jina la Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma na Spika wa Bunge amelipokea na kulisoma mbele ya Bunge na baada ya hapo Bunge wanapiga kura ya kumthibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu.

Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, anakuwa Waziri Mkuu wa Tanzania wa 12 tangu Tanzania tulivyopata Uhuru mwaka 1961 na hit ndiyo orodha ya Mawaziri wakuu wa Tanzania.
Mhe. Julius Kambarage Nyerere 1961 1962
Mhe. Rashid Mfaume Kawawa 1962 hadi 1977
Mhe. Edward Moringe Sokoine 1977 hadi 1980 na 1983 hadi 1084
Dkt. Salim Ahmed Salim 1984 hadi 85
Mhe. Joseph Sinde Warioba 1985 hadi 1990
Mhe. John Samwel Malecela 1990 hadi 1994
Mhe. Cleopa David Msuya 1980 hadi 1983 na 1994 hadi 1995
Mhe. Fredrick Tluway Sumaye 1995 hadi 2005
Mhe. Edward Ngoyai Lowassa 2005 hadi 2008
Mhe. Mizengo Peter Pinda 2008 hadi 2015
Mhe. Kassim Majaliwa Kassim 2015 hadi 2025
Mhe. Dkt. Lameck Mwigulu Nchemba 2025-
 
Back
Top