Kasomi
JT Founder
ALIYEJITABIRIA MTANDAONI ATAFARIKI 2025 AJIUA KWA KUNYWA SUMU. “ALISOMESHA MPENZI, KAHUDUMIA MTOTO, AKAACHWA”
Kijana aliyefahamika kwa jina la Justine Nyalusi wa Kata ya Kitisi, Njombe mwenye umri wa miaka 28 ameleta simanzi kubwa kwa familia pamoja na wananchi wa Kijiji chake baada ya kunywa sumu siku ya jumatatu na kufariki jumanne akiwa anaendelea kupatiwa matibabu.
Sababu hasa ya kunywa sumu yaelezwa kuwa ni “stress” za kimapenzi baada ya kuambiwa na mzazi mwenzake kwamba mtoto waliyekuwanaye kwa muda wa mwaka kwamba siyo mtoto wake bali ni mtoto wa baba mwingine.
Kipindi cha uhai wake Justine alijituma kumhudumia mtoto pamoja na mama mtoto akiamini mtoto ni wa kwake, lakini alipoitwa kwenye kikao cha familia ya mama wa mtoto aliambiwa aache kabisa kutoa huduma kwa mtoto, na atarudishiwa gharama zake. Justine alishimdwa kuvumilia suala hilo ndipo alipoamua kuchukua uamuzi mgumu.
Kitu kilichowashangaza wengi zaidi ni kitendo cha yeye mwenyewe kujitabiria kifo kwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook na Instagram kuwa “alizaliwa mwaka 1997 na kufa mwaka 2025. Sababu ya kifo ni familia na mambo ya mahusiano”.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Pumzika kwa amani Justine Nyalusi..