Advertise here

Jinsi ya kuishi Mnapokuwa na Mahusiano ya Mbali

Kasomi

JT Founder
JINSI YA KUISHI MNAPOKUWA NA MUHUSIANO YA MBALI.
1739774725846.jpg

Kiuhalisia hakuna anayependa kuishi na mwenzi wake mbali mbali, mnapokuwa kwenye mahusino ni muhimu mkawa pamoja, lakini kuna muda inatokea maisha yanawatenganisha kwa muda, katika hali hii ni nini mnatakiwa kufanya ili mahusiano yenu yadumu? Tuone mambo kadhaa ambayo mnatakiwa kufanya;

1. AMINIANENI.
Uaminifu ndio nguzo ya kila mahusiano, huu uhusiano hauji tu ila zipo sababu, ni lazima uwe muaminifu kweli ili uaminiwe. Kwa watu walio mbali mbali kitu cha muhimu ni uwazi katika kila jambo unalofanya. Ajue ratiba zako kama unatoka na mambo mengine, sio mwenzako anakupigia simu anasikia upo kwenye gari, anakuuliza unaenda wapi ndio unaanza kutoa maelezo sijui naenda kwa rafiki yangu, sijui naenda wapi, hiyo haifai. Ukiachana na maelezo nengine yote ila unatakiwa kuwa kuaminifu kweli.

2. KUWENI NA MAWASILIANO IMARA.
Tofauti na mahusiano mengine ambayo wao wapo pamoja muda wote, ila nyinyi mnaunganishwa na mawasiliano ya mara kwa mara. Hii itawasaidia kuendelea kuwa na hisia za pamoja muda wote. Msiache ipite siku bila mawasiliano.

3. AMBIANENI CHANGAMOTO ZENU.
Zungumzeni kuhusu hisia zenu, kile mnachopitia kila siku, ambianeni kuhusu huzuni zenu na furaha zenu, kama kuna shida hakikisheni mnajadili suruhisho la hilo. Manapokuwa mbali haimaanishi kuwa unapokuwa mpweke basi utafute mtu wa karibu kumuelezea upweke wako au shida zako, mueleze mwenzi wako.

4. LENGO LENU LIWE MOJA.
Lazima lengo lenu liwe moja, hii itawasaidia kuvumiliana, yani kila mtu anajua kwanini nipo mbali na mwenzangu, na hiyo sababu ya kuwaweka mbali iwe na mashiko.

5. MUWE NA RATIBA.
Mpo mbali mbali kwa sasa iwe muwe na ratiba ya lini sasa mtakuwa pamoja, hamuwezi kuishi hivyo siku zote. Kunapokuwa hakuna ratiba kamili inachosha, yani kutojua lini tutakuwa pamoja ni ngumu kuvumilika, watu huvumilia wanachokijua, kama hakijulikani ni ngumu kuvumilika.

6. EPUKENI MIGOGORO ISIYO YA LAZIMA.
Kama mnaishi mbali mbali halafu mnagombana bila sababu za msingi, vipi mkiishi pamoja? Lakini kubwa zaidi mnapogombana na mpo mbali mbali ni ngumu kutatua hiyo changamoto na hii inaweza kupelekea mahusiano yenu kufifia.

7. OMBENEANENI.
Kama mnaamini katika Mungu basi kumbukaneni katika kuombeana. Hii siraha itawasaidia.

8. WEKENI KUMBUKUMBU NZURI.
Muda mchache mnaopata wa kuwa pamoja jaribuni kufurahia mahusiano yenu, jaribuni kutengeneza kumbukumbu nzuri, kumbukumbu hizi zitawasaidia kuendelea kuwaweka pamoja mnapokuwa hampo pamoja.

9. JIWEKE MBALI NA VISHAWISHI.
Mnapokuwa mbali mbali unakuwa na nafasi ya kufanya chochote unachotaka, ila kwa faida ya mahusiano yako jiweke mbali na kishawishi chochote, vishawishi vitakutumbukiza katika vitu ambavyo vitaharibu mahusiano yako, lakini kubwa zaidi usifikiria unachokifanya kwa siri hakitakuja kufahamika, ipo siku mwenzako atajua, tena katika nyakati zenu nzuri na hapo kila ulichokijenga kwa miaka kingi kitaharibika kwa sekunde moja na hautaweza kujenga tena.

10.JIBORESHE WEWE KAMA WEWE.
Wakati mwenzio yupo mbali na anapigania ndoto fulani na wewe unatakiwa kuendelea na maisha yako wewe kama wewe, fanya kazi zako na mipango yako mingine iende kama kawaida, usikae tu kumsubiri mtu aje, anapokuja akute hatua kutoka kwako.

Kumbuka, mapenzi sio ni kwa jinsi gani mpo karibu au mpo mbali mbali, ila ni kwa jinsi gani kila mtu yupo na huyo mwenzake, jinsi gani mnachukuliana. Unaweza kuwa unalala na kuamka na mtu kila siku ila bado anakusaliti kila siku iitwayo leo, ila mtu anaweza kuwa mbali huko na bado muaminifu kwako. Kila mahusiano ya safari yao tofauti, usijifananishe na wengine, tembeeni katika safari yenu.

Imeandikwa na Doctor Peter Leader.
 

Similar threads

Back
Top