Advertise here

Mtanzania Noel Sebastian, ameunda mfumo wa Akili Unde wenye uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali

Kasomi

JT Founder
Screenshot_20250220-074601~2.png
Mtanzania Noel Sebastian, ameunda mfumo wa Akili Unde wenye uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali kama vile kuwaongoza watu wenye uoni hafifu au wasioona kabisa katika mambo mbalimbali.

Mambo hayo ni pamoja na kuwaongoza katika kusoma na kutembea huku ukielekeza njia za kupita, na kuainisha hatari zilizopo katika mazingira yanayomzunguka mtumiaji wa mfumo huo.

Akizungumza kwenye mahojiano katika Kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1, Noel amesema mfumo huo unafanyakazi kupitia programu yake inayowekwa kwenye simu janja na unaweza kufanyakazi badala ya binadamu katika kuwasaidia watu wenye changamoto ya kuona.

Amesema licha ya yeye kuwa mwanafunzi anayesomea Udaktari wa binadamu, lakini alijifunza mtandaoni namna ya kutengeneza mifumo ya Akili Unde kutokana na kutokuwepo kwa vyuo maalumu vinavyofundisha teknolojia hiyo nchini.

Chanzo: TBC online
 
Back
Top