Kasomi
JT Founder
MOROGORO: Jeshi la Polisi limesema linachunguza tukio la kifo cha Yosia Johani Keya (25) Mwanachuo Mwaka wa Tatu katika Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) baada ya kukutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia shuka alilofunga kwenye Kenchi la Makazi ya Wanachuo upande wa Baraza la Nyuma
Taarifa ya Polisi imeeleza tukio hilo limetokea Machi 9, 2025 asubuhi Kampasi ya Mazimbu, Kata ya Mazimbu, Manispaa ya Morogoro ambapo uchunguzi wa tukio hilo umeanza ili kubaini chanzo cha tukio hilo
Jeshi la Polisi limetoa wito Watu kutumia madawati mbalimbali ya ushauri nasaha na nasihi kueleza changamoto zao badala ya kuchukua Sheria mkononi