Muda hausimami anza leo

Mtata

Member
✍️ RAFIKI, SIKIA HII! ✍️

Hautaamini itakapofika Novemba 2025 na bado haujafanya chochote.

⏳ MUDA UNAKIMBIA!

Muda hausimami kwa ajili yako—haulijali hali yako ya kifedha, huzuni zako, au maandalizi yako. Hata kama umefiwa au umeachwa kweny swala la WAKATI it doesn't matter _It was once January today is March, soon is November_

⚡ KABLA HAUJACHELEWA...

Ndoto unazozifikiria kila siku, mawazo yanayokusumbua kila usiku—anza kuzifanyia kazi SASA HIVI! Akili yako inakudanganya kwamba bado muda upo, lakini ukweli ni kwamba, muda hautakusubiri! 🚫

🎬 Kama unataka kutengeneza content kwenye social media...

Anza leo, hata kama huna vifaa vya gharama! Acha kisingizio cha kamera mbovu 📸, tumia ulichonacho. Nunua tochi kama lighting, tumia simu yako—bonyeza button ya record!

🎵 Kama wewe ni mwanamuziki...

Usisubiri hadi utunge wimbo "mkali" ndio utoe—toa kile ulichonacho sasa!

🎨 Kama wewe ni designer...

Usingoje hadi utengeneze masterpiece mpya—post hata kile kidogo ulichonacho, ujifunze kutoka kwa makosa, na uendelee kuboresha.

🚀 Wakati wengine wanaachia kazi zao, wanajitangaza, wanajifunza kutokana na makosa, na wanazoea soko, wewe unasubiri duka kubwa ndo uanze kuuza?
🔥 AMKA! 🔥

Anza kutafuta wateja leo. Usisubiri pesa nyingi ndo uanze gym. Usisubiri hali iwe "nzuri" ndo uanze safari yako.

⏳ MUDA HAUSUBIRI!
"Aangaliaye upepo hata panda; anayetazama mawingu hata vuna."
Mhubiri 11:4

Chochote unachowaza—ANZA SASA ! 💡

JARIBU HII-Acha simu chukua daftari na KARATASI andika kila wazo linalokuja kichwani mwako then anzia hapo.
 
Upvote 0
Back
Top