Advertise here

Maelezo/Ndodoo Muhimu za Maombi ya Ajira Katika Mfumo; Ajira za Muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi 2022

Kasomi

JT Founder
MFUMO WA MAOMBI YA KAZI ZA UKARANI NA USIMAMIZI WA SENSA

DONDOO ZA MAOMBI YA AJIRA
KARIBU KATIKA MFUMO AJIRA ZA MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022.
MAELEZO/ DODNDOO MUHIMU


1- Soma Tangazo la Ajira kwa umakini, kabla ya kutuma maombi.

2- Hakikisha Taarifa zote unazojaza ni za kwako.

3- Namba ya Simu itatumika mara moja tu. Hakikisha unajaza namba ya simu ambayo haijatumiwa na mtummwingine kufanya maombi ya ajira.

4- Hakikisha barua pepe (email) unayotumia ni ya kwako na inafanyakazi. Barua Pepe itatumika mara moja tu.

5- Baada ya kutuma maombi Pakua Fomu Na. 1 ili ikajazwe na Wadhani Pamoja na viongozii wa serikali ya Mtaa utakapofanyia kazi.

6- Jina la Mtumiaji na Nywila vitatumwa katika barua pepe (email) uliyoijaza hapo juu (Dondoo namba 3).

7- Ili kukamilisha maombi yako, Tumia Barua Pepe na Nywila uliyotumiwa ili kupakia Fomu Na. 1 iliyosainiwa.

Taarifa ninazo hitajika kujazwa kwenye fomu​

(Sehemu zote zenye alama ya * ni lazima kujazwa)

Sehemu A: Taarifa za mwombaji
1- Jina la kwanza
2- Jina la kati
3- Jina la ukoo
4- Namba ya simu
5- Barua pepe
6- Tarehe ya kuzaliwa (Kama ilivyo kwenye cheti cha kuzaliwa)

7- Kiwango cha Juu cha Elimu Ulichofikia
8- Namba ya mtihani kidato cha nne (Mfano:S1234-0012-2006)
9- Namba ya mtihani(Mfano:S1234-1234-2006)
10- Nafasi Inayoombwa (Chagua nafasi moja tu)
11- Uzoefu wa kutumia simu/Kishikwambi
12- Hali ya ajira
13- Namba ya Kitambulisho cha Taifa kama ilivyo kwenye kadi NIDA
Namba ya NIDA (Mfano:19900102-12345-00001-12)

14- Chagua sehemu utakayo fanyia kazi;
1- Mkoa
2- Wilaya
3- Halmashauri
4- Jimbo
5- Tarafa/Wadi
6- Kata/Shehia
7- Kijiji/Mtaa

Sehemu B: Taarifa za wadhamini

1- Majina matatu ya mdhamini wa kwanza
2- Barua pepe ya mdhamini wa kwanza
3- Namba ya simu ya mdhamini wa kwanza
4- Majina matatu ya mdhamini wa pili
5- Barua pepe ya mdhamini wa pili
6- Namba ya simu ya mdhamini wa pili

Sehemu C: Viambatanisho

1- Cheti cha kidato cha nne (PDF)
2- cheti cha kuzaliwa (PDF)
3- Picha (jpeg,jpd,png)
4- Kiambatanisho kingine (Mfano Cheti cha taaluma ya TEHAMA, n.k) PDF {kiambatanishi hiki ni hiyari}

NB: Kwa ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana kwa namba za simu zifuatazo:- 0744820401, 0769716392, 0737904688, 0768122230, 0733333531, 0713599290, 0718906003, 0715271745, 0716388335

Soma Tangazo Hapa
 
Mi mfumo umenikataa cjui umehisi nitakua ngoswe????????????????????????
Umesoma vigezo vyote kwa umakini???. Soma TANGAZO rudia mara nne mpaka mara tano ikiwezekana uwe na peni na karatasi unachukua important notes baada ya kuelewa vizuri vuta pumzi muombe mungu andaa nyaraka zako vizuri na wadhamini hakiki taarifa zako Soma TANGAZO tena mara ya mwisho pumzika baada ya masaa kaza Anza applications. Acha pupa
 
Back
Top