Kasomi
JT Founder
Familia ya Hayati Rais John Pombe Magufuli ikiongozwa na Mtoto wa Dr. Magufuli aitwaye Jesca Magufuli, imeongoza maandamano ya amani jana March 16 2025 Chato, Geita kumuenzi Hayati Magufuli na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza na kukamilisha miradi iliyoanzishwa na Hayati Magufuli.
Maandamano hayo ambayo Mgeni rasmi wake alikuwa ni Rehema Sombi Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa (UVCCM) yalifika hadi Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato kutoa msaada kwa Wanawake waliojifungua pamoja na wale Wajawazito na kuchangia damu.
Matembezo hayo yaliongoza mamia ya Vijana yalikwenda pia mpaka kwenye kaburi la Hayati Magufuli lililipo nyumbani kwake Chato ambapo wamefanya Ibada ya kumuombea Hayati Magufuli, ibada ambayo pia imehudhuriwa na Viongozi wengine wa UVCCM kutoka Mtwara, Arusha, Kigoma na Geita.
Dr. John Pombe Magufuli ambaye alizaliwa October 29, 1959 alifariki dunia March 17,2021 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ambapo alizikwa kwenye makaburi ya Familia nyumbani kwake Chato ljumaa March 26,2021.
Tazama pia
Historia ya Dkt John Pombe Magufuli
WASIFU WA JOHN POMBE MAGUFULI Taaluma yake; Dkt, John Joseph Pombe Magufuli ni mwalimu na mtalaamu wa kemia akiwa na Shahada ya Uzamivu (PhD). Kuzaliwa Alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1959 huko Katoma tarafa ya Bugando wilayani Geita jimbo la Geita vijijini. Kipindi hicho Geita ikiwa ni moja ya...
jamiitalk.com