Advertise here

Muhtasari wa Hoja: Madhara Ya Kutosaini Kanuni Za Maadili ya Uchaguzi

Kasomi

JT Founder
MUHTASARI WA HOJA: MADHARA YA KUTOSAINI KANUNI ZA MAADILI YA UCHAGUZI

Anaandika Faida Potea✍️

1. Maadili ya Uchaguzi ni Suala la Kisheria

Yameainishwa katika Kifungu cha 162 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, 2024.

Tume ya Uchaguzi hutunga kanuni hizo kwa mashauriano na vyama vya siasa na Serikali, kisha huzichapisha kwenye Gazeti la Serikali.

2. Nani hupaswa kusaini?

Sheria inahitaji kila chama cha siasa, kila mgombea, Serikali na Tume kusaini.

Mgombea anapaswa kusaini kabla ya kuwasilisha fomu ya uteuzi.

3. Wakati wa Kusaini ni Upi?

Sheria haijaweka muda mahsusi kwa vyama au Serikali kusaini.

Kwa mantiki hiyo, chama kinaweza kusaini wakati wowote kabla ya kuanza kampeni.

4. Tafsiri ya “Kusaini” Kisheria

Neno “ kusaini ” halijapewa tafsiri finyu; linaweza kumaanisha pia kuridhia au kukubaliana kwa namna yoyote rasmi.

Mgombea anaridhia kanuni zilizopo, hata kama hajasaini moja kwa moja.

5. Madhara ya Kutosaini

Sheria haijaeleza adhabu au athari ya moja kwa moja kwa chama au mgombea asiyesaini.

Haki ya kushiriki uchaguzi ni ya kikatiba na haiwezi kuondolewa kwa kutokuwepo saini ya kanuni.

Kifungu 162(2) kinaelekeza waliotia saini kuzingatia kanuni, lakini hakielezi kuhusu wasiosaini.

Hii inaacha mwanya wa kisheria (lacuna) unaoweza kutumiwa na baadhi ya wadau.

6. Hitimisho

Sheria hii ina utata na inaweza kuleta sintofahamu katika utekelezaji.

Kukataa au kushindwa kusaini hakumaanishi kufutwa kwa haki ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi.

Haki inaweza kuondolewa tu kwa msingi ulioelezwa wazi na Sheria au Katiba, si kwa tafsiri au hisia.

Mimi faida potea naomba kueleweshwa kwani Mimi nimeona hii hoja imenyoka wewe unasemaje
 
Back
Top