Kasomi
JT Founder
WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema Wananchi, wataruhusiwa kupiga picha au kurekosi video katika Daraja la JP Magufuli (Kigongo–Busisi) lakini ni lazima kuomba kwanza kibali rasmi kutoka Wizara ya Ujenzi.
Waziri Ulega amezungunza hayo leo Alhamisi, Juni 19, 2025 jijini Mwanza katika hafla ya uzinduzi wa daraja hilo iliyoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
“Hatutakataza kufanya kazi zozote za kijamii kama vile kupiga picha au kurekodi kwaya, lakini ni muhimu kuomba kibali kutoka wizara ya ujenzi. Tuna Meneja wa Tanroads atakayeshughulikia utoaji wa vibali hivyo,” amesema Waziri Ulega
Chanzo; Kitenge TV