Babalevo apeta Tatu Bora Ubunge Kigoma Mjini ndani ya CCM!
Mchakato wa kuwania tiketi ya CCM kugombea Ubunge wa Kigoma Mjini umechukua sura mpya! Awali wagombea walikuwa 9, lakini baada ya mchujo wa awali ngazi ya wilaya, majina ya Kilumbe Shaban, Baruan Muhuza (mtangazaji maarufu) na Dkt. Ahmed Sovu ndio yaliyopitishwa.

Lakini mambo yalibadilika ghafla mara baada ya kufikishwa ngazi ya mkoa! Kamati ya Siasa ya CCM mkoa wa Kigoma ilifanya uchambuzi upya na kuchukua maamuzi ya kushangaza—kumtoa Dkt. Sovu na kumrejesha Baba Levo kwenye orodha ya tatu bora!

Sasa Kilumbe Shaban, Baruan Muhuza na Baba Levo ndio majina yatakayowasilishwa kwa hatua za juu zaidi za chama, ambapo mmoja wao atateuliwa rasmi kuwa mgombea wa Ubunge Kigoma Mjini kwa tiketi ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025!

Unaona nani anastahili kupeperusha bendera ya CCM Kigoma Mjini ambapo ataenda Kuchuana na Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo na Wagombea Wengine katika UchaguziMkuu ili kuliongoza Jimbo hilo ?