Kasomi
JT Founder
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, amefanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu aachie wadhifa huo wiki iliyopita, akikosowa vikali jinsi chama tawala cha mapinduzi, CCM, kilivyokiuka utaratibu kwa kumpitisha mgombea urais wa Tanzania na Zanzibar, huku akitaja historia yake ya utumishi mpaka hatua aliyofikia.
Polepole amesema hakukubaliana kabisa na uamuzi wa CCM kuwapitisha wagombea urais hao mapema mwaka huu katika kikao ambacho hakikuwa na majukumu hayo huku akijisifia kwamba amekuwa karibu na serikali tangu mwaka 2000 na ameshiriki katika masuala mengi ambayo baadhi yalimfanya aende katika majukwaa mbalimbali ya kimataifa.
"Na hapa nitawasema, wale wanaokuwaga wenyeviti wa kamati za maadili wanajua... Hili ni gumu kidogo.. unajua wakati mwingine unatakiwa ubomoe ili ujenge. Sasa, huu mchakato wa kupata wagombea kwa kweli tumeukosea, nimeongea na mzee mmoja, ndugu yangu, rafiki yangu nikamweleza, akasema pale bwana tulichemka.. Lakini sasa tunatokaje? Nikamwambia, kukiri tatizo ni sehemu ya suluhu.. nendeni mkarekebishe, mkipatie heshima chama chetu..." alisema Polepole.